HABARI ILIYOTIKISA JIJI-BEI YA UMEME IMESHUKA RASMI,EWURA YASEMA KUSHUKA ZAIDI YA HAPO,KAULI YA PROFESA MUHONGO YATIMIA SOMA HAPA KUJUA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo |
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza kushusha
bei ya Umeme nchi nzima toka shilingi 257.3 kwa uniti moja hadi 251.70 kwa
uniti moja ni sawa na asilimia
2.21.Anaripoti KAROLI VINSENT.Endelea nayo.
Kushuka huko kwa Umeme
imekuja siku chache kupita baada ya Waziri wa Nishati na Madini George
Simbachawene kuitaka Mamlaka hiyo kushusha bei ya umeme kutokana na nishati ya
Mafuta kushuka bei kwenye masoko mbalimbali hapa nchi na Duniani.
Akitangaza Bei hizo mpya
za Umeme leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari ,Mkurugenzi
mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za nishati na Madini(EWURA) Felix
Ngamlagosi ambapo amesema Mamlaka hiyo baada ya kuangalia vipengele vitatu
ambavyo vinafanya umeme kupanda bei ikiwemo-
Bei ya Mafuta katika soko la
dunia,hali ya shilingi ya kimarekani pamoja na mfumo wa gharama za umeme kwa
ujumla wamebaini shirika la Umeme nchini TANESCO,linahaja ya kupunguza Umeme.
Ngamlagosi amezitaja bei
hizo mpya ni kwa wateja wenye matumizi ya kawaida ambao wanaotumiza zaidi ya uniti 7o kwa mwezi,bei
ya umeme itashuka kutoka 306 kwa uniti
hadi 298 kwa uniti sawa na punguzo la shilingi 8.
Na kwa wateja wanaotumia
uniti 70 tu kwa mwenzi bei yao itabaki palepale ya shilingi 100 kwa uniti kama
ilivyokuwa mwanzo.
Bwana Ngamsagosi
alizitaja sehemu zingine ambazo ni kwa
wateja wa viwandani ambao wanatumiza zaidi ya Volti 4oo,kwa mwezi bei ya umeme
imeshikuka kutoka shilingi 205 kwa uniti
hadi 200 kwa uniti sawa na punguza la shilingi 4 kwa uniti,
Mbali na hao wateja
wengine ni wale waliounganishwa na msongo mkubwa wa umeme,bei ya umeme itashuka
kutoka Shilingi 159 kwa uniti hadi 156 kwa uniti ambayo nao ni sawa na punguzo
la shilingi 3 kwa uniti.
Aidha,Bwana Ngamsagosi
alisema Bei hizi zitaanza kutumika Rasmi tarehe moja ya mwezi wa tatu mwaka huu.
Vilevile amesema kuwa bei
hiyo ya umeme itapungua zaidi baada ya kukamilika kwa Bomba la gesi kutoka
mtwala hadi Kinyerezi linalotarajia kumalizika mwezi wa sita mwaka huu,
Mbali na Bomba na Gesi Bwana Ngamsagosi alisema Shirika la Umeme Nchini
Tanesco ambalo linatarajai kuzima mitambo yake yote ya mafuta ambayo ni ya
dharula nayo pia itasaidia kushuka kwa umeme.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni