MAANDAMANO YA CUF,KOVA AIBUKA SHUJAA,LIPUMBA AUFYATA SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Kamishna wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman kova picha na maktaba |
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuthibiti maandamo ya Jumuiya
ya Vijana wa Chama Cha wananchi (JUVICUF) yaliyopangwa kufanyika leo Jijini Dar
es Salaam, baada ya mwenyekiti wa Chama hicho profesa Ibrahimu Lipumba kukubali
yaishe.Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kufanikiwa huko kwa Jeshi la Polisi
kuthibiti maandamano hayo kunamaliza Vita iliyotangazwa jana na mwenyekiti wa
JUVICUF ambaye alitangaza maandamano kuanza makao makuu ya chama hicho zilizopo
Buguruni Jijini hapa hadi ofisi za
wizara ya mambo ya Ndani zilizopo Posta , huku wakijanadi hawatamuogopa Polisi
yeyote.
Akithibitisha kuthibiti maandamano
Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova leo wakati wa mkutano na
Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,ambapo Kamishna Kova huku akiongea kwa
madaha amesema Jitahada za jeshi la hilo
la polisi wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuthibiti maandamano hayo kutokana
Jitahadi kati yake Kamishana Kova na Mwenyekiti wa CUF profesa lipumba baada ya kuona maandamano hayo
yataharibu amani ya nchi.
Kanishna Kova ameongeza kuwa baada ya
kufanya mawasiliano na Profesa Lipumba na kuongea nae kwa mda mrefu huku wote
kwa pamoja wakizungumzia madhara ambayo yatatokea baada ya maandamano hayo
kufanyika,ndipo Profesa Lipumba akabaini maandamano hayo yatakuwa na madhara
makubwa ikiwemo kuleta machafuko pamoja na vurugu .
Aidha,Kamishna Kova amesema kuwa hali ya Amani katika Jiji la Dar es Salaam sio nzuri kufanya maandamano na pindi jeshi la polisi linapozuia maandamano hayo
hawafanyi kwa ajiri ya kuzorotesha siasa nchini bali wanafanya hivyo ili
kurinda amani ya nchi ambayo inaweza kuharibika kwenye maandamano hayo.
Alibainisha, kuwa kwa sasa maandamano na
mikutano yenye lengo la kuvuruga amani hayatakubalika na hivyo jeshi la polisi
litalazimika kutumia uwezo wake wote wa kisheria kuyadhibiti kwa mbinu
mbalimbali.
Vilevile Kamishna Kova aliwashukuru
Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho
Profesa Lipumba kuonyesha Busara ya hali ya juu baada ya kubaini kwamba
kufanyika maandamano hayo yangesababisha madhara makubwa ikiwemo umwagikaji wa
damu na wakati mwengine kwa watu ambao hawahusiki na usumbufu huo.
PROFESA LIPUMBA ANENA.
Naye
mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu lipumba akiyahahirisha
maandamano hayo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari makao Makuu ya chama
hicho yaliyopo Buguruni leo Jijini Dar es Salaam aliwataka wanachama wa chama hicho popote walipo kuacha
kufanya maandamano hayo kutokana na kubaini kuwa kutakuwa na uvunjifu wa Amani.
Maoni 1
Kichwa cha habari kinapotosha yaliyomo katika taarifa yenyewe. Kamanda Kova anasema kuwa mwenyekiti wa CUF amefanya busara na ametoa maelezo ya kuwa walifanya mazungumzo ya kina. Lakini kichwa cha habari hakionyeshi uungwana wala adabu. Jirekebisheni.
Chapisha Maoni