CHUO CHA USAFIRISHAJI "NEEMA TUPU", SASA KUANZA KUKAGUA MAGARI YOTE NCHINI,
Mkuu wa chuo cha usafirishaji, Eng Zacharia Mganilwa wakitiliana saini na Kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango Tanzania, Bw. Joseph Masikitiko mapema hivi karibuni. |
Chuo cha taifa cha usafirishaji sasa kitaanza zoezi lake la kukagua magari yote hapa nchini ambayo hayakukaguliwa na shirika la viwango hapa nchini katika kituo chake cha ukaguzi wa magali kilichojengwa ndani ya chuo hicho Jijini Dareslaam,
Wakitiliama saini na kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango TBS, Mkuu wa chuo cha Taifa cha usafirishaji amesema Hatimaye dhamira ya serikali kuhakikisha inaondoa gari mbovu barabarani sasa itatimia kufuatai cho chake sasa kuanza kufanya kazi ya kukagua magari yote kabla hayajaanza kutumika katika barabara zetu,
Mkuu huyo wa chuo ameongeza kusema kuwa, ukitoka hapa kwenda mikoani kwa mfano Mbeya, humo barabarani utakutana na misululu ya magari mabovu na hiyo ni kutokana na vituo vya ukaguzi wa magari kabla ya kuanza kutumia barabara zetu kutokamilika,
Hivi sasa tayari chuo cha taifa tumejenga uwezo wa kukagua magari zaidi ya mia nne kwa siku lakini kwa kuanzia tunaanza na line moja ambayo inauwezo wa kukagua zaidi ya magari 100 kwa siku na hivyo tunahakika tutapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani,
Aidha katika hatua nyingine mkuu huyo wa chuo, amewataka wazazi kuchangamkia fursa ya kufundisha watoto wao katika kozi ya VIHECLE INSPECTION inayotolewa chuoni hapo kwani kozi hiyo inawigo mpana wa kupata kazi,
Amesema taifa kwa sasa linahitaji watu wa kukagua magari na chuo pekee ambacho kinatoa mafunzo hayo ni NIT hivyo kuna haja ya wazazi kuchangamkia fursa kabla soko halijajaa,
Tunampango wa kufungua matawi nchi nzima ili kukagua magari , sasa lazima tuwe na watendaji kazi , kwa vyovyote vile wale ambao wanasoma kozi hii ndiyo watakuwa kipaumbele cha kwanza na sifa nyine ni ziada tu.
Leteni watoto wenu kwani kozi hii ni bora na gharama zake ni nafuu mno
Kwa upande wake, Kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango TBS Bw. Joseph masikitiko amewaasa wakuu wa chuo cha taifa kutokata tamaa kwa kelele ambazo zitapigwa na watakaotaka huduma chuo hapo hususani hiyo ya kukaguliwa, na hiyo ni kutokana na ukweli kuwa mara zoezi litakapoanza kutakuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau lakini amewataka kutokata tamaa wakaze buti ili ajali za barabarani ziweze kupungua kwa kuondoa magari mabovu .
Najua kutakuwa na kelele nyingi sana lakini usikate tamaa Bw. Mganilwa, watu watasema kituo hakina uwezo, mara muda mwingi unatumika kukagua gari moja lakini uskate tamaa, kwani jambo lolote linaloanza lazima litakuwa na changamoto zake Aliongeza Masikitiko.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni