NEC YAKIRI SASA BVR KULETA MATOKEO MAKUBWA KATIKA MBIO ZA URAIS, WASEMA UMEONESHA MATOKEO MAKUBWA KATIKA MAENEO AMBAYO WAMEFANYA MAJARIBIO
Mwenyekiti wa tume hiyo ,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizngumza na wanahabari mapema leo juu ya zoezi hilo
Tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania NEC imesema kuwa
sasa Tanzania inaweza kutumia mfumo mpya wa uandikishwaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura wa BVR kutokana na mfumo huo kuonyesha mafanikio makubwa baada
ya kuufanyia majaribio katika maeneo kadhaa nchini.
Na Exaudi Mtei
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam
mwenyekiti wa tume hiyo ,Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa tume hiyo
ilifanya majaribio ya kutumia mfumo huo mpya wa uandikishwaji katika majimbo
matatu ambayo ni KAWE,KILOMBERO NA KATAVI ambapo mfumo huo ulionyesha kufanya kazi kwa
uhakika na kujiridhisha kuweza kuutumia katika zoezi la nchi nzima mapema mwaka
huu.
“Tunasema kuwa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa
sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya wapiga kura waliojitokeza
kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo waliyokadiriwa kuandikishwa”amesema
lubuva
Katika takwimu zinaonyesha kuwa kwa mkoa wa dar es
salaam kata ya bunju wapiga kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na kata
ya mbweni wapiga kura 6200 walianndikishwa kati ya 8278,mkoa wa morogoro kata
ya ifakara kakingiuka ipangala,na viuwanja sitini wapiga kura walioandikishwa
ni 19,188 wakati makisio yalikiuwa watu 17,790 na mkoa wa katavi halmashauri ya
milele kata ya ikuba,usevya na kibaoni wapiga kura walikuwa 11,210
walioandikishwa wakati makisio yaklikuwa
watu 11,394 ambapo amesema kuwa
matokjeo hayo yanaonyesha ni jinsi gani wananchi wamekuwa na muamko wa kutumia
mfumo huo na vifaa hivyo vilifanya kazi vizuri.
Aidha jaji LUBUVA amesema kuwa zoezi hilo kwa nchi
nzima litaanza mapema kwani daftari hilo ndilo litakalotumika katika kuipigia
kura katiba mpya katika kura ya maoni pamoja na uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka
huu.
Pamoja na hayo jaji LUBUVA amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo pindi lityaka[poanza nchi nzima kwa
lengo la kujiandikisha katika daftari hilo kwani litawasaidia katika kuipigia
kura katiba mpya na uchaguzi mkuu ujao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni