Zinazobamba

HIVI NDIYO BODABODA DAR WALIUKARISHA MWAKA KWA KUWAONA MAJERUHI HUKO MUHIMBILI, MAKONGORO MAHANGA AWASIFU NA KUSEMA KUWA HILO NI JAMBO JEMA


Msemaji wa wanabodaboda wa kanda ILALA Bw. Abdalah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema hivi karibuni kuhusu kilio chao cha bodaboda kuruhusiwa na kutambuliwa kuwa hiyo nayo ni kazi kama kazi zingine zilivyo, Jumla ya wanabodaboda mbalimbali kutoka Teme, Ilala, na Kinondoni waliungana kwenda kuwajulia hali majeruhi walioumia kwa bodaboda huko muhimbili




Naibu waziri wa ajira, Mh. Makongoro Mahanga akifafanua jambo mbele ya wanahabari mara baada ya kumaliza kuwajulia hali wagonjwa wa bodaboda mapema hiyo jana, Makongoro alitumia fursa hiyo kuwataka madeareva hususani wa bodaboda kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani kwani ajali nyingi zilizoelezwa na wagonjwa zilionyesha uzembe wa madereva
Hapa walikuwa wanajiandaa kwenda muhimbili na gari hili kwenda kuwajulia hali wagonjwa
Maandamano ya wanabodaboda wakiingia katika hospitari ya muhimbili mara baada ya kuanza safari yao toka Mnazi mmoja wakiongozwa na Mh. Mahanga.


Bodaboda wakishusha Zawadi ambazo wamewapelekea wagonjwa huko muhimbili, Hakika bodaboda nayo ni kazi kama kazi nyingine

Dk wa muhimbili akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, Dk. huyo amesema majeruhi wengi wanaopokelewa hapo wanasema wanaumia kwa bodaboda, ni zaidi ya asilimia 54. kwa usiku mmoja tu wa mwaka mpya jumla ya majeruhi 14 walipokelewa huku majeruhi 7 wakiwa ni wa bodaboda.

Hakuna maoni