Zinazobamba

KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA DARESALAAM KUSHEREHEKEA MIAKA 50 TOKEA KUANZISHWA KWAKE, MOKIWA AWATAKA WAUMINI KUHUDHURIA KWA WINGI JUMAPILI HII

Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Daresalaam akifafanua jambo mbele ya mwandishi wa habari wa mtandao huu mapema hii leo kuhusiana na maadhimisho ya miaka 50 ya dayosisi hiyo yatakayofanyika katika makao makuu ya kanisa hilo yaliopo posta. Katika maadimisho hayo mgeni rasmi anategemewa kuwa waziri wa mambo ya nje Mh. Benard Camirius Membe

Askofu mokiwa akiwa anafafanua dhaidi kuhusu maadhimisho hayo muhimu, katika maadhimisho hayo kutakuwa na mambo mbalimbali yakiwemo ya makongamano ya vijana na michezo mbalimbali. Mokiwa amewataka waumini wa kanisa hilo na wasio waumini wajitokeze kwa wingi ili kusheherekea pamoja mafanikio ya dayosisi ya Dareslaa kwa  kufikisha miaka 50

Na magali
Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dareslaam, linatarajia kuazimisha miaka hamsini ya utumishi wake mapema jumapili ambapo askofu wake mkuu wa dayosisi hiyo ametumia fursa hiyo kuwataka waumini wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi kwenda kuanzimisha miaka hiyo hiyo jumapili,

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo katika makao makuu ya dayosisi hiyo yalioko Ilala kona ya Arusha na Moshi, Mokiwa amesema kuazimisha miaka hamsini hiyo ni faraja kwa kanisa kwani katika miaka hiyo 50 kunachangamoto mbalimbali ambazo kanisalimepitia
Askofu Valentine Mokiwa ametaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuhudumia jamii katika mazingira magumu hususani katika sekta ya afya ambayo mpaka sasa wanajitahidi kuhakikisha kuwa wanajenga vituo vingi kadri wanavyoweza ili kuleta huduma bora kwa waumini wao na jamii ya kitanzania kwa ujumla,
Aidha akizungumzai maadhimisho hayo ya miaka 50 ya dayosisi ya Daresalaam, Mokiwa amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na makongamano mbalimbali ya vijana, michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa wavu, basketi ball, na michezo mingine,
Aidha akizungumzia maadhimisho hayo kwa undani zaidi, Mokiwa amesema, maadhimisho hayo yatawaleta waumini wa kanisa hilo karibu na viongozi na hivyo kuondoa ile dhana ya kuchangamana kati ya viongozi na waumini wao,
Aidha Askofu mokiwa ametaja baadhi ya mafanikio ambayo dayosisi hiyo wameyapata katika kipindi hicho cha miaka 50, na kusema kuwa wamefanikiwa kuwa na vitega uchumi mbalimbali ikiwemo shule mbalimbali za nusery, za msingi.
Amesema, katika mikakati yao ambayo wameipanga ni kuanza kuwa na kinywa cha kanisa ambapo wamesema kanisa lifungua kituo cha redio ili waumini wake waweze kupata taarifa sahihi za kanisa kupitia chombo chao,
Na katika kuhakikisha kuwa dhamira yao hiyo nzuri inafikiwa, kanisa limeamua kuchangisha fedha kupitia taasisi mbalimbali kama vile za sumatra na zinginezo ili kuwa na fedha za kuanzisha kituo hicho

Hakuna maoni