HABARI ILIYOTIKISA JIJI-WAZIRI MWAKYEMBE AFUKUZA KAZI MABOSI TRL,ATOA MACHOZI MBELE YA WAFANYAKAZI SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa Shirikala la reli (TRL) leo jijini Dar es Salaam |
NA KAROLI VINSENT
HUKU ikiwa imebaki Miezi kumi ili Rais Jakaya Kikwete amalize
mada wake,Sasa WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameidisha Cheche Baada
ya leo Kuibuka na kuwasimamisha pamoja na kuwafukuza kazi watumishi 12 wa Kampuni la Reli Tanzania (TRL), kwa tuhuma za
kuhujumu shirika hilo huku akiagiza wachukuliwe hatua za kisheria pamoja na kufulisiwa.
Hatua hiyo ni mwendelezo wa Waziri Mwakyembe kusafisha
wafanyakazi wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu, vinavyokwenda kinyume na
jitihada za serikali kutaka TRL kujiendesha kwa faida na kuondokana na
utegemezi ambao shirika hilo limekuwa mzigo kwa sasa kwa serikali kutokana na
ufisadi huo.
Akizungumza na
waandishi pamoja na wafanyakazi wa TRL,Mda huu Jijini Dar es Salaam ,ambapo Waziri Mwakyembe aliwataja wafanyakazi
waliofukuzwa kazi ni Stanley Makunja, Stanley Edward, Jason Moses, B. Luoga, Edward
Benedict, na Lucy Ntinya ambapo wanadaiwa kugushi malipo ya tiketi za abiria na
kuitia hasara TRL.
Wafanyakazi wa Shirika la Reli nchini pamoja na Waaandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Waziri Mwakyembe |
Alisema wafanyakazi
hao waligushi malipo ya tiketi za abiria waliokuwa wakisafiri na treni kwenda
mikoa mbalimbali nchini ambapo malipo waliolipa abiria hao ni tofauti na malipo
yaliyoandikwa kwenye kitabu cha risiti.
Mwakyembe aliongeza kuwa wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti waligushi
risiti mbalimbali zikiwemo zenye namba 622405 iliyolipiwa sh. 50,200 lakini
fedha iliyoingia TRL ni sh 13,600, risiti yenye namba 6224010 iliyolipiwa sh
74,400 huku fedha iliyoingia kwenye kampuni hiyo ni 13,600
Aidha ,Mwakyembe
alitaja risiti yenye namba 622408 iliyolipiwa sh 57,000 ilighushiwa huku TRL
ikipata sh 6,700 hivyo alisema kitendo kilichofanywa na wafanyakazi hao
hakikubaliki.
Vilevile, katika
mkutano huo, alitangaza kusimamishwa kazi maafisa sita wanaodaiwa
kuiisababishia hasara kampuni hiyo kwa kushindwa kuhakiki ubora wa mabehewa ya
maizigo yaliyonunuliwa na serikali.
Waziri Mwakyemba Aliwataja
maafisa hao ambao ni waandisi kuwa ni Pascal, Ngoso, Kaukunda, Chambika, Lugela
na Kessy ambapo barua zao za kusimamishwa kazi wamekabidhiwa Disemba 10 mwaka
huu.
Alibainisha kuwa
pamoja na maamuzi hayo kufikiwa, bodi ya zabuni ya TRL imevunjwa na tayari
mchakato wa kuundwa kwa bodi mpya umeanza.
Katika sakata hilo
la ubovu wa mabehewa ya mizigo na kusababisha kuanguka pindi yanapokuwa
safarini, Mwakyembe ameunda kamati ya wataalamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), Bodi ya
Wahandisi, TRL huku akimuagiza Katibu
mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kuongeza wataalamu wawili kufuatilia ubora wa
mabehewa hayo.
Mwakyembe ambaye
pia ni mbunge wa kyela CCM,Alisema kamati hiyo itakwenda nchini India kwenye
kampuni ya Hindu Stant kuhakiki ubora wa mabehewa hayo na pindi ikibainika kuwa
hayakutengenezwa kulingana na viwango vinavyokubalika basi serikali itachukua
hatua za kisheria,
“ Lazima tukahakiki ubora wa mabehewa hayo kwakuwa inashangaza
kuona mabehewa mapya pekee ndiyo yana anguka hivyo lazima tufahamu ukweli wa
mambo” alisema.
Katika hatua nyingine
Mwakyembe aliitaka bodi ya TRL kusitisha mikataba na kampuni za Translaw, R and
A works, Solar security, Kigema security na Intergrated zilizokuwa na mikataba
na TRL.
Alisema kazi
zinazofanywa na kampuni hizo zikiwemo kuhesabu idadi ya mizigo inayosafirishwa
zinaweza kufanywa na wafanyakazi wa shirika hilo.
Alisisitiza kuwa
madai yanayotolewa na Menejimenti ya TRL kuwa kazi hizo zinahitaji uwepo wa
wafanyakazi wengi na wenye ujuzi mbalimbali ikiwemo za ukarani, na ukarabati wa
miundombinu ya reli hayana msingi.
Aidha,Mwakyembe
alisema kwa upande wa kampuni za ulinzi ni vyema kazi hiyo ikafanywa na SUMA
JKT shirika kwa kuwa wanauwezo wa kuhakikisha vitendo vya wizi vinadhibitiwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni