MKESHA WA MWAKA MPYA,KAMANDA KOVA AAPA KUFA NA MTU,NI YULE ATAKAYEVUNJA SHERIA SOAMA
Pichani ni Kamishana Suleiman Kova picha na Maktaba |
NA KAROLI
VINSENT
Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam limepanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba
mkesha kuelekea Mwaka Mpya 2015 unakuwa salama na amani na Jeshi hilo alitosita
kumchukulia mtu ama vikundi vyovyote vilete uvunjifu wa Amani.
Onyo hilo limetolewa Leo Jijijini Dar es Salaam na Kamanda wa Kanda
Maalum ya polisi Kamishna Suleiman Kova wakati wa Mkutano na Waandishi na
Wahabari ambapo alisema sherehe za mwaka mpya, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wachache hasa vijana hupenda
kuchoma matairi barabarani, kulipua fataki na vurugu za kila aina kwa lengo la
kuonyesha furaha yao ya kuingia mwaka 2015.
Hali kama hiyo haitavumiliwa na Jeshi
la Polisi kwa sababu badala ya sherehe hugeuka vitisho, vurugu, na kisha
kuwatia hofu wananchi wasiokuwa na hatia. Katika harakati hizo Jeshi limeweka
mpango kazi utakaowashirikisha askari wa vikosi vyote pamoja na wadau
mbalimbali watakaojihusisha na ulinzi siku hiyo. Watakaojihusisha na ulinzi ni
pamoja na kikosi cha Zimamoto, kampuni binafsi za Ulinzi, na katika Jeshi la
Polisi kutakuwa na kikosi cha FFU na kikosi cha Mbwa na Farasi.
Kamishna Kova aliongeza kuwa Kampuni binafsi za Ulinzi zitashiriki
kikamilifu katika ulinzi huo ambapo watafanya doria za miguu kwa pamoja, doria
za magari, pamoja na askari wa pikipiki. Kwani Baadhi ya watu hupenda
kusherehekea mwaka mpya katika nyumba za ibada ambapo Jeshi la Polisi litatoa
ulinzi.
Kamishna kuva alitaja aini ya ulinzi
utakao tumika ni ulinzi katika fukwe za bahari pamoja na sehemu zote ambazo
zinzkuwa na mikusanyiko ya watu wengi kama vile katika Hotel kubwa kubwa na sehemu
za wazi. Uwanja wa Taifa utalindwa kutokana na mikusanyiko mkubwa wa watu
utakaokuwepo siku ya mkesha pamoja na viwanja vingine vyote vyenye mikusanyiko
mingine kama hiyo.
Vilevile,Magari ya Zimamoto
yatafanya doria yakisindikizwa na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kwamba yeyote
atakayejaribu kuchoma moto matairi au gari atakamatwa na moto unazimwa.
Kutakuwa na ulinzi wa
kutosha ufukweni mwa bahari ambapo Boti za Polisi zitafanya doria ili kuwabaini
wahalifu wa aina yoyote kutoka Baharini au nje watakaojaribu kuingia na kufanya
uhalifu jijini.
Helkopta ya Polisi itaanza doria
kuanzia saa kumi na mbili jioni ili kukagua maandalizi yoyote ya uchomaji moto
au uhalifu mwingine wa aina yoyote. Wananchi wanashauriwa kuwa makini na
familia zao na hasa watoto wadogo wasiruhusiwe kuingia barabarani wakati wa
sherehe hizi kwani ni hatari kwa maisha yao
Kamishan Kova alitoa
wito kwa Watanzania kutoa taarifa kwa viongozi wa Polisi pale watakapoona
Viashiria Vyovvote vya uvunjifu wa amani kwa kupiga namba hizi
wananchi kwa jumla kutoa taarifa wakati ambapo kuna ishara ya uvunjifu
wa amani au wakiwaona watu wanaowatilia mashaka watoe taarifa kwa namba
zifuatazo:
1. ZCO - Constantine Masawe – SACP: 0713-510
856 / 0658-111 100
2. RPC ILALA – Mary Nzuki – SACP: 0715-009 980 / 0754-339 558
3. RPC TEMEKE – Kihenya Kihenya – SACP: 0715-009 979 / 0754-397 454
RPC K’NDON– Camillius
Wambura – ACP: 0715-009 976 / 0684-111
111
Hakuna maoni
Chapisha Maoni