MAUAJI MAHAKAMANI LEO,HABARI KAMILI HII HAPA,NI UZEMBE MKUBWA SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Askari wakimtoa Mtuhumiwa wa madwa ya kulevya aliyekuwa akitaka kuwatoka Akari ambapo jeshi hili lilimpiga risasi |
NA KAROLI
VINSENT
KATIKA hali
isiyokuwa ya Kawaida Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Imegeuka Uwanja wa Damu
baada ya Mtuhumiwa wa Dawa za Kulevya aliyetaka kuwatoroka Kizembe Maaskari wa
Jeshi la Magereza Nchini na Askari hao kumrushia Risasi na kupelekea Kifo chake.
Tukio hilo la Aina yake limetokea Leo mapema
Katika Mahakama hiyo ya Hakimu mkazi Kisutu iliyoko jijini Dar Es Salaam.
Wakilizungumzia Tukio hilo la Aina yake ,Mashuhuda
walioshuhudia hali hiyo waliozungumza na Mtandao huu wamesema Ilipofika majira ya Saa 2.30 asubuhi
Gari la magereza likiwa limewabeba wafungwa lilifika Salama Mahakamani hapo.
Pichani ni Mtuhumiwa Huyo |
Ambapo Waliposhuka wafungwa wengine
Vizuri, ila ilipofika zamu ya Mfungwa huyo aliyepigwa Risasi ambae jina lake
halikuweza kupatikana mara moja alishuka salama,mara akawaomba Ruhusa Askari wa
Magereza waliokuwa wakitoa ulinzi mahakamani hapo ili aende Kwenda kujisaidia Chooni
wakati aliporuhusiwa kwenda , Mara Gafla Mtuhumiwa huyo akaanza kuwatoroka
kizembe Askari na kuanza kukimbia ili
kuwatoroka Askari hao mapaka kwenye ukuta uliozunguka Mahakama ya Kisutu ili
kutoroka.
Ndipo Askari wa Magereza waliokuwa
wakitoa ulinzi kwa wafungwa wakamrushia Risasi ambayo ilimpata kwenye Mguu
licha risasi hiyo kumapata hapo lakini bado
Mtuhumiwa huyo wa madawa ya Kulevya alikuwa bado anaendeleo kupanda ukuta ili
kutoroka,Askari hao wakarusha Risasi nyingine ndio ikampata kwenye Paji la Uso
na kupelekea kifo chake kama picha zinavyoonyesha.
Akilizungumzia Tukio hilo Mwanasheria wa Kujitegemee ambaye
alilishuhudia tukio hilo huku akikataa kutaja jina lake Mtandaoni alisema “Huu ni Uzembe wa hali ya Juu wa jeshi la
Magereza waliounyesha leo katika kuwarinda wafungwa maana aingii akilini kabisa
mtuhumiwa anashuka harafu apewi ulinzi wowete,ndio maana tunalia sana majeshi
haya waajiri watu wasomi waache mazoea”alisema Mwanasheria huyo.
Naye Askari wa Magereza aliyezungumzia
Tukio hilo kwa Masharti ya kutotaja jina lake kwa Mwandishi wa mtandao huu
alisema
“Tatizo tunafanya Kazi kimazoea sana
haiwezekani kabisa Mfungwa asimamiwe kieenyeji vile,na hili linatushusha hazi
kazi yetu kwa ufanyaji kazi wa hali hii,yaani tukio hili limenishangaza sana”alisema
Alipotafutwa kamanda wa Polisi wa Kanda
Maalum Kamishna Suleiman Kova kuhusu
Tukio hilo alisema hawezi kulizungumzia suala kwa madai sio mamlaka yake kutoa
ulinzi kwa wafungwa na akawataka waandishi wangojee taarifa kamili kutoka kwa Jeshi
la Magereza nchini.
Mtandao huu ulipojalibu kuwatafuta Viongozi
wa Jeshi la Megereza ili kuzungumzia tuhuma za Uzembe wa Askari wa Magereza hao
mpaka mtuhumiwa huyo kuwatoroka, juhudi hazikuweza kuzaa matunda kutokana na
simu zao zote kutopatikana,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni