HABARI KUBWA LEO-SIRI YA KUFUKUZWA MWIGAMBA,PROFESA MKUMBO YAFICHUKA,NI DHAMBI YA USALITI WA CHADEMA YAWATESA TENA,BOFYA HAPA
Aliyekuwa Katibu mkuu wa chama cha ACT TANZANIA--SAMSON MWIGAMBA ambaye amefukuzwa kutokana mikakati ya kukihujumu chama chama hicho picha na Maktaba |
NA KAROLI
VINSENT
TAMAA ya
madaraka,kukosa uvumilivu wa mambo ndio kunakowaponza Wanasiasa Profesa Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba hadi kupelekea kufukuzwa
kwenye chama cha Siasa cha ACT –Tanzania.MTANDAO HUU UNARIPOTI.
Profesa Mkumbo na Samson Mwigamba wote
wawili kabla ya Kuhamia ACT-Tanzania walitokana na Kufukuzwa Chadema kwasababu ya kendesha mipango ya kuupindua Uongozi wa Mwenyekiti
wa Chadema Freeman Mbowe ulioijenga Chadema kimafaniko makubwa.
Pichani ni Profesa Kitila Mkumbo |
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao
huu umezipata zinasema Kilichomponza Profesa kitila na Samsoni Mwigamba ambaye
ni pia ni katibu Mkuu wa ACT-Tanzania hadi kufukuzwa kwenye chama hicho ni kutokana na kuandaa
mipango ya kutaka kumpindua Mwenyekiti wa sasa wa ACT-Kadawi Limbu katika
nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali zinasema
lengo la wawili hao ni kumpindua mwenyekiti wa Chama hicho Bwana Limbu katika nafasi hiyo
ili-
Mwanachama mwenzao aliyefukuzwa na
Chadema Zitto Kabwe ashike nafasi ya Limbu.
Zitto,ambaye ni mbunge wa Kigoma
kaskazini,alifukuzwa Chadema yapata mwaka Mmoja sasa,na tangu hapo amekuwa
akifahamika kuwa mwanzilishi au “mwanachama wa kimyakimya” wa ACT
“Umoja huu kati ya Profesa Kitila na
Mwigamba umelenga kukiua chama chetu na sisi hatutokubali lazima
tuwafukuze,maana tunajua viongozi hawa wameunda umoja eti kupambana Limbua
aondoke ili wamelete huyo Zitto na sisi hatubali”alisema Kiongozi Mwanzilishi
wa chama hicho ambae akutaka jina lake litajwe.
Chanzo kingine kinasema kuwa Shaaban Mambo
ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho
amekuwa akisema “Limbu ni mwenyekiti Boya na kwamba mwenyekiti halisi
anatarajiwa kuwasili mapema mwaka huu “
Wakati
kundi moja likijipanga mipango ya kumsimika Zitto,nao kitila na Mwigamba
wanadaiwa kuitisha Kikao cha kamati kuu chenye lengo la kuwafukuza wale ambao
watapinga “Ujio” wa Zitto.
Mtoa Tarifa Mwengine anasema “Mwigamba
ameitisha Kikao kinyume na katiba .yeye na wenzake wamepanga kuutumia mkutano
huo kuwafukuza baadhi ya viongozi wakiwemo Mwenyekiti wa sasa na wale
wasiokubaliana nao”
Amesema Mwigamba na Kitila wanataka
kuteka ACT na kugawa wanachama kama walivyofanya chadema na sisi hatutokubali
kwani wataka kumtoa Limbu wamkabidhi Zitto kabwe.
“Hatukubali kukiacha chama
tulichokipigania kifie mikononi mwa Wahamiaji,tumejipanga kukabiliana nao”
Wengine wanaotarajiwa kufukuzwa na
kwenye chama ili kumasafishia njia Zitto Kabwe
ni Naibu katibu mkuu (Bara) Leoold Mahona,Katibu mwenezi na mwenyekiti wa Vijana Taifa,Grasyon Nyakarungu na Ramadhani
Suleiman Ramadhani ambaye ni makamu Mwenyekiti (Zanzibar)
Wapo
pia,Mselemu Suluhu,naibu katibu mkuu Zanzibara na Dotto Zakayo
Wangwe,Mwenyekiti wa Wanawake Taifa.
Naye mchambuzi wa Siasa na Msomi kutoka
Chuo Kikuu huria cha Tanzania Martin Kileo alisema kitendo wanachofanya wakina
Mwigamba na wenzake hakikubaliki.
“Hawa
watu ni wauni tu hawana nia ya kuikomboa siasa za nchi,huyo Profesa Mkumbo ni
mamluki tu anatumiwa na chama Tawala kuja kuvibomoa vyama vya Siasa na ACT wasiokubali kuyumbishwa na hawa
watu”
Maoni 1
taarifa yako inamapungufu makubwa,kwanza zitto hajafukuzwa chadema bali alivuliwa nyadhifa zake za uongozi akibaki kuwa mwanachama wa kawaida.tafadhali kuwa na uhakika na kile unachokiandika
Chapisha Maoni