Zinazobamba

EXCLUSIVE-MADUDU YA PROFESA KITILA MKUMBO HAYA HAPA,AZIDI KUJIABISHA NA ELIMU YAKE SOMA

Pichani ni Profesa Kitila Mkumbo picha na Maktaba

NA TIMU MAALUM YA MTANDAO HUU
PROFESA Kitila Mkumbo aliyefukuzwa na Chadema  kwa kosa la kuandaa mapinduzi ya kuupindua utawala uliokuwa madarakani ukiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Chadema Freeman Mbowe na kukimbilia chama cha ACT-Tanzania-
       Ambapo pia napo Kafukuzwa tena kutokana na kuanzisha Mipango ya kuupindua uongozi ulioko madarakani ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Tanzania Kadawa Limbu ili kumuingiza kinyemela Zitto kabwe katika nafasi ya Limbu.
         Profesa Mkumbo ambaye ni Mwandishi wa Riwaya Maarufu kwenye magazeti mbalimbali ambavyo sasa anasifika kwa kuandika makala zenye kuwakashifu Viongozi wa Chadema pasipo kuwa na hoja yenye mantiki.
        Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali ambazo mtandao huu umezipata zinasema Profesa Kitila Mkumbo amejiunga kwenye upande wa Wasaka Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM .
       Vyanzo hivyo vya Kuaminika vinasema Profesa Mkumbo ambaye ni Mwalimu Chuo Kikuu cha Mlimani ambapo sasa amejiunga upande timu mahususi iliyoundwa ili kumwezesha Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa kuingia Ikulu.
       Aliyefanikisha Profesa Kitila kujiunga na kundi hilo la Lowasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa aende Ikulu, Apson
       Mwang'onda. Katika makubaliano hayo, Profesa Kitila analipwa posho ya shilingi Milioni Tano(5,000,000/=) kwa mwezi ikiwa ni malipo yake
kutokana na ushauri wake kwa Team ya Lowassa.
Pichani Edward lowassa 
          Pia katika makubaliano hayo, Prof Kitila amepewavitendea kazi ikiwa ni pamoja na simu za kisasa,laptop na tablet na kwamba maslahi yake yatazidi kuboresha kwa kadri matunda ya ushauri wake yatakapodhihiri.
                  Inaelezwa kuwa Lowasa alivutiwa na Mkakati wa Siri wa Mabadiliko wa mwaka 2013 ulioandaliwa na Kitila na kundi lake ambao ulikuwa na lengo la kumjenga Zitto Kabwe Kisiasa ndani ya CHADEMA.Ni kutokana na mkakati huo, ndipo Edward
Lowasa alipompa kazi Apson Mwang'onda ya kuhakikisha kuwa Prof Kitila Mkumbo anajiunga na KUNDI lao kutokana na umahiri alionao wa kutengeneza mikakati ya siri ya kisiasa
        Taarifa zilizopo ni kwamba, Profesa Kitila alifuatana na Lowasa Zanzibar alipodaiwa na makada mbalimbali  kutoa pesa ya shilingi Milioni Moja (1,000,000/=) kwa kila mjumbe wa NEC na shilingi laki tano (500,000/=) kwa kila Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM visiwani humo ambapo rushwa hiyo imetolewa wakati wa mapumziko ya Christmas.
       Taarifa zaidi zinasema kuwa mara baada ya kuingia kwenye kundi la Lowasa, Prof Kitila pamoja na ushauri wake anaotoa kwa kundi hilo, amekabidhiwa jukumu la kumshawishi Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
       Benard Membe kuungana na kundi hilo na kwamba Kitila amekubali jukumu hilo na ameanza kulitekeleza kutokana na uswahiba wake na Membe.
          Hoja aliyoeleza Kitila kwa Membe ni kwamba, ikiwa Membe atakubali kuungana na kundi hilo, watakuwa wamejihakilishia safari ya kwenda Ikulu na kwamba Lowasa ndiye atakuwa              Mgombea Urais na Membe atapewa nafasi ya Uwaziri Mkuu baada uchaguzi.

         Inaelezwa kuwa baada ya Membe kupokea maombi hayo, alishauriana na washauri wake akiwemo Anthon Diallo ambao walifikia makubaliano ya pamoja kuwa Membe asiungane
na kundi hilo kutokana na uchafu wa Lowasa.
          Kwamba ikiwa kutakuwa na ulazima wa Membe kuungana na mwanasiasa mwingine, basi anaweza kuungana na Mizengo Pinda ambaye hana uchafu hasa kashfa za ufisadi. Kwa taarifa hii ni dhahiri kuwa kilichotokea ndani ya CHADEMA ndicho kitakachotokea kwa ACT.

Hakuna maoni