Zinazobamba

CHAMA KIPYA CHA ACT CHAPASUKA VIPANDEVIPANDE,KIGOGO WAKE AULIMA WARAKA MZITO VIONGOZI WA JUU SOMA HAPA KUJUA

Aliyekuwa  Katibu mkuu wa chama cha ACT TANZANIA--SAMSON MWIGAMBA ambaye amefukuzwa kutokana mikakati ya kukihujumu chama chama hicho picha na Maktaba
KAMA ni moshi unatoka ambao utapelekea kuwaka moto basi ni ndani ya Chama kipya cha Siasa cha ACT-Tanzania huu ni waraka ulioandikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama cha ACT-Tanzania –Karama Kaila ni huu hapa
    KUHUSU KINACHOENDELEA ACT.
Kianchondelea ndani chama chetu sikutaka kukizungumzia sababu naamini si vizuri kuzungumza mambo ya chama hususani yanoyohusu migogogoro hadharani na bila ya ruhusa ya vikao, na mbaya Zaidi ukiwa si msemaji wa chama. Kwa ilipofikia, nafikiri nami ni bora niseme, sababu naona kuna upotoshwaji wa makusudi unaofanywa na baadhi yetu ndani ya chama lakini kubwa uelewa wa ndivyo sivyo wa watani wetu na baadhi ya wanachama wenzangu.
Tatizo la ACT linasababishwa na watu wafuatao, Mwenyekiti, Naibu katibu mkuu na Nyakarungu kwa upande mmoja na Katibu, Mwekahazina, Mwanasheria na Mwenezi taifa kwa upande wa pili. Kwa hivyo hapa naweza kusema kuna kundi la Katibu Mkuu na Kundi la Mwenyekiti.
Kundi la Mwenyekiti:
Halitaki uchaguzi ndani wa chama, bali linataka UONGOZI huu wa muda uendelee hadi 2016 na mmoja wao aliandika barua kwa msajili kuomba uongozi wa sasa uendelee hadi 2016. Pamoja na sababu zingine, sababu kuu wanayoitoa kama sababu kutofanya UCHAGUZI ni fedha. Chama hakina fedha ya kufanya zoezi hilo la uchaguzi. Nyakarungu katokea CHADEMA lakini yuko na mwenyekiti huenda sababu walikuwa wote na mwenyekiti katika mchakato wa kuanzisha chama AAC kabla hata ya ACT.
Kundi la katibu mkuu:
Kundi hili linataka uchaguzi ufanyike ndani ya chama kabla ya tarehe 5/5/2015. Sabu tarehe hiyo huu uongozi wasasa unatimiza mwaka mmoja.
Pamoja na sababu zingine, sababu kuu wanayoitoa ni kuwa ni kukidhi matakwa ya kisheria, inayotaka uongozi wa muda usikae madarakani Zaidi ya mwaka mmoja. Kuhusu fedha wanasema zitapatikana endapo tukiwa tayari, kama zivyopatikana tulipokuwa tayari katika operesheni nyingi za chama na zilizogharimu fedha nyingi.
MSAJILI ANASEMAJE?
Ameshajibu ombi la kutaka uchaguzi uhairishwe. AMESEMA hilo haliwezekani na sababu zilizotolewa na waombaji hazitoshi kukiuka matakwa ya sheria.
TATIZO HASA NINI? HOFU?
ACT kimetokana na wanachama waliotoka ADC na CHADEMA. Mwenyekiti wetu wa sasa anatokea ADC, makamu mwenyekti anatokea CHADEMA, katibu anatokea CHADEMA, naibu Katibu anatokea ADC.
CHADEMA ni chama kikubwa kuliko ADC, hivyo kadiri ACT inavyokua na inavyokuwa imara inamaanisha wanachama wengi wa CHADEMA wanazidi kujiunga na ACT. Ndio maana bila shaka yoyote kuwa asilimia Zaidi ya 90 ya wanachama wa ACT wametokea CHADEMA. Ndio maana kinachoendelea ndani ya ACT, CHADEMA inakifurahia sababu inajua ACT inakawenda kupunguza kasi yao.
Ninahisi mwenyekiti wasasa aliyetokea ADC na naibu wake ambaye katokea ADC wanahofu tukienda kufanya UCHAGUZI nafasi hizo watazipoteza kwa watu waliotoka CHADEMA. Hivyo wanaona bora wavute SUBIRA na kupima UPEPO sanjari na kutafuta hila ya kubaki pale walipo.
Pamoja na hayo, hivi wanajua kuwa CHADEMA ilivyo, na ADC ilivyo, ni haitatokea hata siku moja kwa watu waliotoka ADC kuongezeka kiasi cha kuwazidi watu waliotoka CHADEMA? Sanasana nikionacho mimi ni kuongezeka kwa wimbi la watu kuvua MAGWANDA na kuvaa UZALENDO. Kama wanahofu hii, bora waachane na hayo na wajikite katika UJENZI wa CHAMA na wanachama watawapima kwa UFANISI wao na si wapi walipotokea. Mwanasiasa na mwanademokrasia haogopi UCHAGUZI bali hupenda UCHAGUZI. Kwa kulijua hili ndio maana Mwenezi taifa anatokea ADC lakini na yeye anasisitiza uchaguzi ufanyike na yuko tayari apimwe kwa utendaji wake wa kazi.
Pia huenda kundi la akina Mwigamba linataka UCHAGUZI sababu linajua litaendelea kubaki madarakani sababu tu chama kina watu WENGI waliotoka CHADEMA kuliko toka ADC. Pamoja na sababu yao ya kutaka UCHAGUZI ina mashiko, lakini kama kuna hili nyuma ya pazia na kama ikiwa watu toka ADC wanalijua hili, basi ni sawa kiasi wagomee uchaguzi huku wakijipanga kubaki walipo.
Hata hivyo, kwa maoni yangu, ni dhahiri kuwa UCHAGUZI kufanyika ni takwa la kisheria na hatuna hiyari juu ya takwa hili, hivyo basi ni HARAMU MUTLAKI kuwafikiria VIBAYA au kudhani wana lao jambo nyuma pazia watu wanaotaka UCHAGUZI. Sababu haiwezekani hata kidogo MTII SHARIA onekane HABITHI mbele ya MVUNJA SHARIA.
HITIMISHO.
Yanasemwa mengi kwa kiachoendelea ndani ya ACT, wapo watu wengine wanatueletea hadithi za mtumbwi na maneno ya kwenye khanga kama ya mtu na mke mwenziwe.
Niwambie kitu kimoja, Mwigamba anataka uchaguzi ufanyike na Prof Kitila kama mshauri wetu ameshauri UCHAGUZI ufanyike, vyovyote iwavyo lakini Mwigamba ametaka hivi ili chama kitii takwa la kisheria na Prof ameshauri hivi ili chama kitii takwa la kisheria pia.
Watu hawa wawili ni wakorofi toka walipokuwa CHADEMA, ila ukorofi wao unaonekana endapo taratibu, kanuni au katiba ya chama zikikiukwa. CHADEMA walifukuzwa na WAKIUKAJI wa katiba ya CHADEMA kwa maslahi yao, na huku ACT wale wale wakiukaji wa sharia kama WACHADEMA wametangaza kuwafukuza.
SHAKA YANGU SASA, hata huko kufukuzwa kwao ndani ya ACT ni mwendeelezo wa ukiukwaji wa katiba yetu hivyo sitashangaa wakiendeleza hicho kinachoitwa UKOROFI hili kufanikisha lengo lao la kujenga chama tafauti kabisa na CCM na CHADEMA. Mwigamba ni mkorofi, tumfanyeje zaidi ya kumuunga mkono? Binafsi nawaunga mkono katika UKOROFI HUU.

Hakuna maoni