TPDC YAMUUMBUA FREEMAN MBOWE ,NI UJENZI WA BOMBA LA GESI,BOFYA HAPA
Pichani ni Meneja Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Angetile Musomba akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam Picha na Seleiman Magari |
NA KAROLI
VINSENT
SHIRIKA la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeweka wazi gharama za Mradi wa
ujenzi wa Bomba la Gesi asilia kutoka Mkoani Mtwala,songosongo-Lindi na Pwani
hadi Dar ES Salaam,ambapo wamesema mradii
huo unatarajia kugharimu pesa za kimarekani Dola Bilioni 1.2 sawa na fedha za
kitanzania zaidi ya Trilioni 1.2.
Kuibuka huku kwa (TPDC)kumekuja siku
chache kupita baada ya Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe, wakati alipokuwa
akichangia Bungeni Dodoma aliitupia
Lawama Shirika hilo kwa Madai limefanya usiri wa Mkataba wa ke wa Gesi na kupelekea kuwepo na ufisadi wa zaidi
ya pesa za kitanzania Trilioni 1.
Akiweka bayana Gharama hizo za mradi leo jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na
Waandishi wa habari, Meneja Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)
Mhandisi Kapuulya Angetile Musomba
amesema garama za mradi wa bomba hilo ni Dola Bilioni 1.2 ambazo ni sawa na
pesa za kitanzania zaidi ya Trilioni 1.2.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Mradi wa TPDC Mhandisi Musomba |
Kati ya pesa hizo Benki ya Exim ya
China imechangia Asilimi 95 na serikali ya Tanzania alimia 5.
Mhandisi Musomba aliongeza kuwa Kiasi
hicho cha Fedha kinatumika kugharamia maeneo mbalimbali ikiwemo-
Mtambo wa kusafisha gesi asilia ya
songo Songo inayogaramia Dola za kimarekani 151,735000,na mtambo wa kusafisha
gesi asilia wa Mnazi bay pia unagarimu Dola za Kimarekani 197,877,000.
Aidha,Mhandisi Musomba alisema mradi huo
umefikia asilimia 94 katika kukamilika kwake na mradi wenyewe unatarajia
kukamilika kwake Mwezi wa sita mwaka huu.
Mradi huo wa Gesi ukikamilika kwake
utasaidia kuwaletea faida kubwa wananchi ikiwemo katika kupata umeme wa uhakika
,kupanua viwanda,utunzi wa mazingira,upatikanaji wa Ajira,maji safi pamoja na
matumizi ya gesi ambapo Bomba hilo la Gesi litapitia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni