MTANGAZAJI OMARY KATANGA APATA SHAVU JINGINE,NI BAADA YA KUTOKA IPP MEDIA,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mtangazaji Omary Katanga |
NA KAROLI
VINSENT
ALIYEKUWA
Mtangazaji wa kipindi cha Michezo ndani ya Redio one ambaye sasa Mtangazaji wa
Redio mpya ya E.FM Omary Katanga amepata shavu jingine,baada ya kuteuliwa kuwa
Afisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dar es Salam (DRFA).
Awali nafafi hiyo ya Afisa Habari kwenye
chama hicho alikuwa inashikiliwa na
Mohamedi Mwalizo ambaye mkataba wake Umekwesha.
Akitambulishwa leo jijini Dar es Salaam
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari na katibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam Msanifu Kondo alisema kuchaguliwa kwa Katanga katika
nafisi hiyo kumetokana na kutambua mchango wake katika kutoa taarifa kwa umma
ikiwemo na umakini aliokuwa nao.
“Katika kikao cha kamati kilichokaa
tumefikia hatua ya kumchagua Omary Katanga kuwa Afisa Habari katika chama hichi
ili aweze kutupa urahisi wakuwapa taarifa wanamichezo pamoja wapenzi wa mkoa wa
Dar es Salaam”alisema Kondo.
Kondo aliongeza Chama hicho
kinampongeza aliyekuwa Afisa Habari wa chama hicho Mohamedi mwalizo kwa kazi
kubwa aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili na akawataka wanahabari kumpa
ushirikiano Katanga katika kazi
Kwa upande wake Afisa huyo habari mpya
Omary Katanga alishukuru kwa kuchaguliwa katika nafasi na kusema ataitumikia
kwa moyo wote na kuwataka wanahabari wenzake wampe ushirikiano kuboresha mpira,
Kuhusu Mkataba wake na Redio E.Fm ambayo
sasa anaitumikia alisema ataendelea kufanya kazi Redio hiyo kwani aimzuii
kufanya kazi na DRFA.
Kwa upande Mwengine DRFA wamesema kwa
sasa wako katika kozi ya Madaktari wa michezo inayotarajiwa kuanza kuanzia 23
mwezi huu hadi tarehe 27 pia mwezi huu,huku pia kukiwa na kozi nyingine ya
masuala ya utawala na washiriki wa kozi hiyo watakuwa wajumbe wa kamati ya
utendaji wa DRFA na Maafisa wa michezo
wa manispaa watendaji
Hakuna maoni
Chapisha Maoni