HABARI KUBWA-ALIYEISALITI CHADEMA ASHUSHIWA KICHAPO,NI SAMSON MWIGAMBA,DHAMBI YA USALITI YAZIDI KUMTESA,SOMA HAPA KUJUA
Pichani Aliyekwidwa ni katibu mkuu wa Mda wa chama cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba jana |
NA KAROLI
VINSENT
SAMSON
Mwigamba aliyefukuzwa ndani ya chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema
kutokana na kuandaa mipango ya kutaka kuupindua uongozi wa Chadema,na
kukimbilia kwenye chama kipya cha Siasa cha ACT-Tanzania na pia huko kaandaa
mgogoro mzito na viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Kadawi limbu ambapo
sasa wamefukuzwa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida jana
katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
ambapo Samson Mwigamba kuchezea kichapo kutoka kwa makundi yanayopingana ndani ya Chama cha
ACT-Tanzania, tukio hilo lilimkuta wakati Mwigamba alipotoka kwenye kikao cha Usuluhishi wa makundi
hayo
Mwigamba ambaye pia ni Katibu
Mkuu wa mda ndani ya ACT-Tanzania inadaiwa ghafla walitokea vijana wanaodaiwa
kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbu na kumvamia
Vurugu hizo zimetokea ikiwa ni siku
chache baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kumsimamisha uongozi Limbu na
kumwondoa katika nafasi yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa
makosa ya kinidhamu.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza
na Mwandishi wa Mtandao huu wanasema sababu ya Mwigamba kuvamiwa inatokana na
kumtapeli kiongozi mwezake wa Chama hicho mkoani Arusha milioni moja .
Bado anakunjwa tu na makada wenzake wa ACT-Tanzania |
Alipotafutwa Mwigamba na Chanzo changu
kimoja huku akizungumza kwa uchaungu alidai
vijana hao wamekodiwa na Limbu kwa lengo la kumfanyia
vurugu baada ya kuona mikakati yake imekwama ndani ya chama.
“Limbu alikuja na kundi la vijana kama 12, kati yao wawili aliwasafirisha kwa ndege kutoka Arusha na mmoja anaitwa Gerald Emmanuel, pia alikuwamo Mwenyekiti wa Geita, Katibu Uenezi Ukonga, Katibu Uenezi Jimbo la Kinondoni pamoja na kina Mahona.
“Limbu alikuja na kundi la vijana kama 12, kati yao wawili aliwasafirisha kwa ndege kutoka Arusha na mmoja anaitwa Gerald Emmanuel, pia alikuwamo Mwenyekiti wa Geita, Katibu Uenezi Ukonga, Katibu Uenezi Jimbo la Kinondoni pamoja na kina Mahona.
Gafla akatokea kiongozi mwengine wa ACT-Tanzania kuja kumgombelezea |
“Sasa wakati bado hatujaingia ofisini kwa msajili tukaambiwa tunatakiwa mimi na Limbu tu ndio tuingie na wengine waondoke, lakini kikundi cha Limbu hakikuondoka wakabaki pale nje wanajadiliana,” alisema Mwigamba.
Alisema wakati wamemaliza kikao na msajili, alifuatwa na Gerald huku akimshika shati lake na kumwambia anamdai fedha zake Sh milioni moja, hivyo lazima amlipe.
Wakatokea Viongozi wengine wa ACT-Tanzania ambao wanamdai wakaanza kumshushia kichapo |
“Wakati tunatoka kikaoni nikawa pale nje nasubiri gari linichukue, akaja Gerald huku akishika shati langu akidai ananidai shilingi milioni moja na lazima nimlipe pale pale, nilishangaa sana na hapo ndiyo nikajua kuna kitu Limbu amefanya ili wale vijana wanivuruge na baadaye nikasirike na kuonekana nimepigana,” alisema Mwigamba
Baada ya Tambwe hizo za mwigamba
zisizokuwa na ushahidi wa moja kwa moja,chanzo changu kilimtafuta na Mwenyekiti
wa chama hicho cha ACT-Tanzania Kadawi limbu
aliyefukuzwa na Ghiriba za Mwigamba na wezake alisema-
hakuona vurugu hizo kwani wakati huo
alikuwa anazungumza na simu pembeni, na kwamba Gerald na Mwigamba wanajuana kwa
kuwa wote wanatoka Arusha.
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, alisema hakushuhudia fujo hizo na kusema kwamba kuna watu wanataka kuvuruga mazungumzo yake na ACT.
“Kuna watu wanataka kuyavuruga haya mazungumzo, ndio haohao ambao wanasambaza hata picha huko kwenye mitandao ya kijamii na kukuza mambo,” alisema Jaji Mutungi.
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, alisema hakushuhudia fujo hizo na kusema kwamba kuna watu wanataka kuvuruga mazungumzo yake na ACT.
“Kuna watu wanataka kuyavuruga haya mazungumzo, ndio haohao ambao wanasambaza hata picha huko kwenye mitandao ya kijamii na kukuza mambo,” alisema Jaji Mutungi.
Kuibuka kwa Mgogoro katika chama hicho inadaiwa kuwepo viongozi wawili
wa chama hicho wakiongozwa na Profesa Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba wote
kwa pamoja walifukuzwa chadema kutokana na Usaliti na kukimbilia katika chama
cha ACT-Tanzania ambapo sasa wameupindua uongozi uliopo sasa.
Kwa mujibu wa
Taarifa mbalimbali zinasema lengo la wawili hao ni kumpindua mwenyekiti
wa Chama hicho Bwana Limbu katika nafasi hiyo ili-
Mwanachama mwenzao
aliyefukuzwa na Chadema Zitto Kabwe ashike nafasi ya Limbu.
Zitto,ambaye ni mbunge wa Kigoma kaskazini,alifukuzwa Chadema yapata mwaka
Mmoja sasa,na tangu hapo amekuwa akifahamika kuwa mwanzilishi au “mwanachama wa
kimyakimya” wa ACT
“Umoja huu kati ya Profesa Kitila na Mwigamba umelenga kukiua chama chetu na
sisi hatutokubali lazima tuwafukuze,maana tunajua viongozi hawa wameunda umoja
eti kupambana Limbua aondoke ili wamelete huyo Zitto na sisi hatubali”alisema
Kiongozi Mwanzilishi wa chama hicho ambae akutaka jina lake litajwe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni