Zinazobamba

HABARI KUBWA-WALIOISALITI CHADEMA WAJUTA, WASEMA NI BORA WANGEBAKI CHADEMA NI WALE WALIOKIMBILIA ACT,VIONGOZI WAKUU WATIMULIWA CHAMA HICHO SOMA HAPA KUJUA


Katibu mkuu wa ACT-TANZANIA ndugu SAMSON MWIGAMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam kuhusu maamuzi ya mkutano mkuu wa chama hicho na yanayoendelea ndani ya chama hicho
NA KAROLI VINSENT
          KATIBU mkuu wa Chama cha kipya cha Siasa cha Alliance for change and Transparency ACT-Tanzania Samson Mwigamba amejikuta akijutia uamuzi wake,baada ya kusema ni bora angebaki Chama cha  Demokrasia na Mandeleo Chadema kuliko chama alichokuwepo sasa cha ACT-Tanzania kutokana na kuwepo kwa viongozi wenye ufinyu wa mawazo.
        
           Samson Mwigamba ambaye alifukuzwa Chadema kutokana na kuandaa mipango ya kuundoa uongozi ulioijenga Chadema Kimafinikio chini ya Freeman Mbowe, na kukimbilia chama Cha ACT-Tanzania ambapo sasa kumeibuka mgomgoro wa Uongozi ndani ya Chama hicho.
       
           Kauli hiyo ya  imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu huyo wa Chama cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema ni bora angebaki kwa kamanda wa anga ambako ni Chadema kuliko wapambanaji wa ardhini ambao ni viongozi wa chama hicho kichanga cha siasa cha ACT-Tanzania.
       
          Mwigamba aliongeza kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa mda wa ACT-Tanzania Kadawi Limbu kuitisha mkutano mkuu ambao tayari uliokuwa na mapungufu kikatiba na kuwatimua Viongozi mbalimbali ambao yeye akiwemo amesema ni   ishara tosha ya kiongozi huyo kuwa kigegeu na mwenye kuwa na kila ishara ya kutumika .    
Shaban Mambo makamu mwenyekiti bara akizungumza
             “Maamuzi yaliyofanywa na Ndugu Limbu hayana uhalali wa kisiasa ,kikatiba na sheria na yalilenga kuwasaidia baadhi ya ,mahasimu wa kisiasa wa ACT-Tanzania  kuonyesha kwamba mimi na wenzangu tuliofukuzwa chadema  ni watu wakorofi na kwamba ilikuwa sahihi kwa Chadema kuchukua hatua wakati tulikuwa tunadai haki na usawa”alisema Mwigamba
      
           Mwigamba alibainisha kuwa kitendo cha Mwenyekiti Limbu kumwandikia  Msajili wa Vyma vya Siasa nchini kumuomba uchaguzi wa ndani kwenye chama hicho ufanyika mwakani 2016 ni ishara ya kiongozi huyo anaogopa uchaguzi ndani ya c hama na pia alivunja katiba ya namba 5 ya  msajili wa vyama vya siasa.

          “Sheria za msajili ziko wazi nashangaa huyo mwenyekiti limbu anazivunja ikiwemo sheria namba 5 ya msajili wa vyama vya siasa nchini inasema “Uongozi wa muda utabaki na uhalali wake kwa muda ya miezi 12  tangu kupata usajili wa kudumu kama unavyoeleza  na sheria za vyama vya siasa,nashangaa sasa huyu mwenyekiti wa mda anafanya utoto huu wa kuongeza tena miezi 12 mengine ambayo ni kinyume na taratibu”aliongeza Mwigamba.         
Mwanasheria wa chama hicho THOMAS MATATIZO akisoma maazimio ya chama juu ya viongozi waliovunja taratibu
   Maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

         Akisoma maazimio ya Mkutano mkuu uliofanyika mapema wiki hii  Jijini Dar ES Salaam na kuhudhuliwa na wajumbe 11 kati ya 22.
Akisoma Maazimo ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuhusu Viongozi hao walidiriki kuwafuza viongozi mbalimbali mbali wa chama hicho,Mwanasheria wa chama hicho THOMAS MATATIZO alisema Mkutano huo mkuu umefikia hatua ya kumwondo mwenyekiti wa ACT-Tanzania Kadawi Limbu ambaye amevunja kanuni na sheria ya chama hicho.
Wanahabari kazini
        “Kwa kuzingatia mamlaka yake ya kikatiba (Ibara ya katiba 27 (c),kamati kuu imemsimamisha ndugu  Kadawi limbu, huku Naibu Katibu mkuu bara Leopold Mahona atachukuliwa hatua kwenye mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ambao ndiowenye mamlaka ya uteuzi wake”aliileza Mwanasheria huyo

Hakuna maoni