Zinazobamba

WAKAGUZI WA MIGODI WAELEZWA UMUHIMU WA CHECKLIST KATIKA UKAGUZI


unnamed 
Washiriki wa kikao kazi cha kuandaa miongozo (checklist) ya ukaguzi wa migodi wakiwa katika makundi kujadiliana namna ya kuandaa miongozo hiyo.
unnamed1 
Baadhi ya Wakaguzi wa migodi wakiwa katika majadiliano kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi.
unnamed3Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel Baraka akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.

unnamed5Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha kuandaa checklist ya wakaguzi wa migodi wakiwa katika kazi za vikundi kuandaa miongozo hiyo.
………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Mwanza Imeelezwa kuwa, wakaguzi wa migodi wanao mchango mkubwa katika kuepusha ajali zinazotokea migodini hususani kwa wachimbaji wadogo endapo watatoa mapendekezo na maoni yatakayowezesha kuandaa miongozo (checklist) itakayotumika katika ukaguzi wa migodi. Hayo yameelezewa na Mtaalamu kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Noel Baraka wakati akitoa mada katika kikao kazi cha wakaguzi wa migodi wanaokutana kwa lengo la kuandaa checklist zitakazotumika kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa migodi. Akizungumzaia hali halisi ya watalaamu hao, alieleza kuwa, bado kuna upungufu wa wakaguzi wa migodi huku idadi kubwa ikiwa ni watalaamu wachanga ambao bado hawana uzoefu wa kutosha katika shughuli hizo. “Pamoja na upungufu huu lakini endapo tutaandaa checklist nzuri itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha ajali migodini,” ,alisisitiza Baraka. Wakati huo huo, akitoa mada katika kikao hicho, Mhandisi Assa Mwakilembe amewataka wakaguzi hao kuzingatia maeneo muhimu mbalimbali ambayo yameainishwa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yakiwemo masuala ya uhifadhi wa mazingira, usalama na afya na kuwataka wataalamu hao kutoa kipaumbele katika maeneo hayo wakati wa shughuli za ukaguzi wa migodi nchini. Vilevile, akitoa mada ya namna ya kuandaa miongozo ya ukaguzi (checklist), Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje ameeeleza umuhimu wa kuwa na checklist katika shughuli za migodi kwamba, zitawezesha kufahamu mapungufu yaliyoko migodini na hivyo kujua namna bora ya kutoa ushauri wafanyapo ukaguzi katika migodi ya wachimbaji wakubwa na wadogo.

Hakuna maoni