Zinazobamba

LHRC, CHADEMA WAMKABA KOO HAWA GHASIA, WASEMA LAZIMA AJIUZURU.... MWENYEWE AGOMA AMTUPIA ZIGO JK


Wanaharakati wamemtaka waziri ghasia kung'oka katika nafasi yake kutokana na kushindwa kusimamia watu wake na hivyo kupelekea kuharibu kwa mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mtaa, kwa kuwa na dosari nyingi huku halmashauri tatu zikishindwa kufanya chaguzi.
Hayo yamebainishwa leo na Harold Sungusia ambaye alikuwa anazugumzia jinsi walivyoutazama uchaguzi huo wao kama waangalizi wa ndani na kusema kuwa ni uchaguzi ambao umejaa matatizo matupu ambayo ni haki kama Ghasia akawajibika ili matatizo kama haya yasije yakajirudia
 Wakili Harold Sungusia amesema wao kama waangalizi wa ndani ambao walipewa jukumu la kuangalia uchauzi huo na ofisi ya waziri mkuu wamebaini kuwa uchaguzi huo umeghubikwa na wimbi la uzembe wa hali ya juu ambao haupaswi hata kufumbiwa macho, Sungusia amesema, kuna sehemu watu wanakuta majina yao tayari yametumika , huku yeye mwenyewe akiwa hajapiga kura na hivyo kupelekea watu wengi kushindwa kupiga kura kwa uzembe huo,


Ukiachiliambali tataizo hilo bado watanzania wengi wamekuwa ni wahanga kwa kushindwa kupiga kura kwa tatizo tu la kuchanganya nembo na majina  ya wagombea kitu ambacho kwa watu walio makini hata kidogo kisingeweza kutokea
Kituo hicho ambacho kilikuwa kinafuatilia uchaguzi huo kwa mara ya kwanza kwa kutumia TEHEMA,amesema hakika tehama imewasaidia sana katika kupata taarifa muhimu ambazo zimewawezesha kujua uchafu ambao uliokuwa ukifanywa na watumishi ambao wamepewa dhamana ya kusimamia uchaugizi huo ambao ni muhimu sana kwa mustakabali wa wakazi wa mitaa, kitongoji , vijiji na taifa kwa ujumla,
Kituo hicho kimeshauri, mkuu wa msafara ambaye pia ni waziri wa Tamisemi ajiuzuru kwa kushindwa kusimamia uchaguzi huu ambao kwa hakika anasema umeharibiwa makusudi,

Hata hivyo, Waziri mwenye dhamana na Tamisemi Tayari amejibu tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa kwake kwa kusema kwamba yeye kama waziri kwa ngazi yake amefanya vizuri kwani katika halmashauri zote nchini ni halmashauri Tatu tu ndo zimefanya vibaya,
Ghasia amesema amejipima na kugundua kuwa yeye katika ngazi ya kitaifa bado wamefanya vizuri na ndio mana halmashauri nyingi zimefanikiwa kwa asilimia miamoja lakii kwa zile ambazo zimefanya vibaya ndyo hizo wameamua kuzichukulia hatua kali za kinidhamu,
Mimi katika ngazi yetu siwezi kujiuzuru kwa sababu tumefanya vizuri, labda kama RAISI JAKAYA M. KIKWETE akiona kama hajaridhishwa na utendaji kazi wangu basi atachukua hatu lakini ninahakika kuwa nimefanya vizuri na haw ambao wameenda kinyume nimepeleka majina yao na raisi amekubali kutengua ukurugenzi wao,

Aidha Ghasia ameenda mbele na kusema kuwa watanzania lazima wajue kuwa serikali yao ipo makini na haitamuonea aibu mtu yeyeote ambaye ataenda kinyume na maadili ya ongozi,
kuhusu hatua ambazo hawa ghasia amezichukua soma http://fullhabari.blogspot.com/2014/12/habari-iliyotikisa-jiji-rais-kikwete.html

CHADEMA WAIBUKA NA HOJA ZA KUTETEA WAKURUGENZI
Huku hali ikiwa hivyo kwa kituo chasheria na haki za binadamu, Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kupitia katibu mkuu wake Zanziba, Mh. Salum Mwalimu wameibuka na kusema kuwa wanajiuliza mara mbili ni kwanini wakurugenzi ambao wamechukuliwa hatua ni wale ambao halmashauri zao ndizo chama cha chadema kimefanya vizuri???? na kuhoji kulikoni,
Akizungumza na Fullhabari mapema hii leo Katibu huyo amesema wanashangwa kuona waziri mwenye dhamana ameibuka na kuwachukulia hatua wakurugenzi ambao chadema ndio wamefanya vizuri kuna siri gani hapa na ni kwa nin
Mwalimu anasema kwa vyovyote vile Chadema kupitia mwanasheria mkuu wake, Ndg. Tundu Lissu watafuatilia kwa makini sakata hilo ili kuweza kujilizisha na tuhuma ambazo wakurugenzi ambao wametupiwa virago, kama ni za kiuonevu basi chadema haitasita kuwasimamia hadi hapo haki yao inapopatikana
kwa sasa wawe wapole tunaliangalia suala hili kwa jicho la pili na kama itagundulika kuwa wakuu hawa wameonewa kisa Cchadema amepita katika maeneo yao basi hatutakubali mtu kuonewa na haki itachukua mkondo wake

Hakuna maoni