Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI:SAKATA LA ESCROW LHRC WAMTAKA PINDA KUFUTA KAULI YAKE,

HAROLD SUNGUSIA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO.
 Wakati joto la kashfa ya ya wezi wa mabilioni ya shilingi kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow bado halijapowa, wanaharakati wa kituo cha sheria na haki za binadam wameibuka na kumtaka waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kufuta kauli yake ya kuwadanganya watanzania kuwa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow si za umma,

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, Mkurugenzi  wa utetezi na maboresho ya sera wa  LHRC WakiliHarold Sungusiaamesema kituo chake kinaona ni vema mkuu huyo wa nchi kuwaomba radhi watanzania kwa kufuta kauli yake kwani taarifa zote muhimu zinaonyesha wazoi kuwa fedha hizo ni za umma,


Ameendelea kusema kuwa, ofisi kuu za serikali ikiwemo ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali, ofisi ya Takukuru na kamati ya PAC ameonesha kwa kila hatua kuhusu ukweli kuwa fedha hizo ni za umma na kupendekeza hatua stahili zichukuliwe kwa watuhumiwa ambao kwa namna moja ama nyingine wamefdaidika na account hiyo,

Sungusia ameongeza kusema kuwa, kwa wabunge ambao kwa namna moja ma nyingine walionekana kuutetea uongo kuwa ukweli ni vyema nao wakachunguzwa na kuangalia kama kuna mazingira ambayo yanaonyesha kuwa wamechukua rushwa basi ni vyema na wao wachukuliwe hatua,

Tunaamini huenda kunabaadhi ya wabungewamehusika katika sakata hili la Escrow na ndio maana hata spika wa Bunge ana makinda aliwanya wabunge wake kuacha maramoja tabia ya kupokea rushwa kwani watashindwa kuisimamia serikali ipasavyo, na kama hivyo ndivyo basi tunadhani ni vyema basi bunge lichunguze na kama kuna waliohusika na kashfa hii hatua za kisheria zichukuliwe
Aidha katika hatua nyingine kituo hiko cha sheria na haki za binadamu wamepongeza jitihada ambazo wabunge wamezifanya katika kuhakikisha kuwa wanaisimamia serikali, hususani kwa hatua yao nzuri waliyoifkia ya kutoa mapendekezo ambayo yanamaslahi kwa taifa,

Sungusia amesema maazimio ambayo bunge wameyafikia ni mazuri na ambayo kwa hakika yanapaswa kuigwa kwani kila mmoja wetu ameridhishwa na maamuzi yale na kwamba sasa kazi imebaki kwa muhimili mmoja wa serikali ambao wanatarajiwa kuyatendea haki maadhio hayo ya bunge ambayo hata wananchi wanayakubali kwa asimilimia zote

Naye HAMIS MKINDI ambaye ni Afisa Program dawati la
uangalizi wa Bunge na uchaguzi hakusita kuonyesha hisia zake kwa kusema kuwa kwa mara ya kwanza bunge la Tanzania limeweza kufikia makubaliano kwa kipindi cha dakika 45 ambazo kwa hakika wametoka na majibu mazuri na kuhoji hivi ni kwa nini maamuzi kama yale hayakuweza kufikiwa katika sakata la uundaji wa katiba pendekezwa???????
Wakati wa kuunda katiba pendekezwa kulikuwa na kutofautiana kwa mitazamo, lakini bunge lilishindwa kufikia makubaliano ambayo yalipelekea hadi leo watu kugawanyika na katiba inayopendekezwa,
Anasema busara ambayo imetmika hapa nayo ingetumika kule katika bunge la katiba mambo huenda yangekuwa mazuri sana aliongeza Bw. Hamisi Mkindi


Aidha katika hatua nyingine kituo kimeshauri kuwa kauli iliyotolewa na Makinda kuhusu bunge kuhongwa isipuuzwee hata kidogo

Kituo kimesema kuwa hoja hizi kuwa kuna baadhi ya wabubge sio wasafi ni hoja nzito na hazifai kupuuzwa na kupitwa hivi hivi hivyokituo chao kinazitaka mamlaka zinazohusika kuanza uchunguzi mara moja kujua kama kuna wabunge waliofanya kitendo hicho na wakipatikana waunganishwe katika sakata la ESCROW kwani nao ni wezi mali za watanzania. 

Aidha kituo hicho kimelitaka bunge kuichukulia kwa uzito wa aina yake kauli hiyo ya spika ili kama kuna baadhi ya wabunge waliochukua pesa ili kutetea wezi wa pesa za escrow wawachukulie hatua za kinidhamu wabunge hao.
Mbali na kauli aliyoitoa spika MAKINDA vile vile mbunge wa sikonge mh SAID MKUMBA akichangia katika mjadala ule pia alisikika akisema kuwa “Nasikia kuna watu wanapita pita wakigawa fedha mbona kwangu hawapiti”kauli ambayo inawapa wasiwasi wananchi kuwa kuna baadhi ya vitendo vya rushwa ndani ya bunge ili kuwaficha waovu ndani ya bunge.

Katika mjadala uliomalizika wiki jana ulishuhudia baadhi ya wabunge wakibishana kwa maneno huku wengine wakijaribu kutetea kile ambacho kinaitwa ni wizi wa wazi wa hela za account ya tegeta ESCROW huku wengine wakitaka wahusika wawajibishwe.
 
Katika hatua nyingine LHRC wameipongeza kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali chini ya mwenyekiti wake mh ZITTO KABWE kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi hapa walipofikia ni kazi kubwa na wanapaswa kupongezwa kwa kuwafichuo watu wanaotafuna mali za watanzania.

Hakuna maoni