SAKATA LA MAUAJI YA WANAWAKE DAR-KAMANDA KOVA AMALIZIA UBISHI KUHUSU MAUAJI HAYO-SOMA HAPA KUJUA
Na Karoli
Vinsent
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam
limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu
kwa kufanya vitendo viovu vya utekaji, unyanyasaji kijinsia na mauaji ya
wanawake.
Watu hao ni ABUBAKARI
S/O AMANI @ KASANGA, Miaka 28, Mkazi wa Mwenge na EZEKIEL S/O KASENEGALA @ VALATANGA, Miaka 25, Mkazi wa Tandika
jijini Dar es Salaam.
Akithibitisha kuwakamata wahalihu hao Mda huu Jijini Dar
es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari ,Kamishna wa Kanda Maalum ya
Dar Es Salaam Suleiman Kova ambapo alisema Watuhumiwa hawo wamehusishwa na
vitendo hivyo baada ya upelelezi wa kina na wa kitaalam ambao umesaidia
kuwakamata wahalifu hao wakiwa na vielelezo mbalimbali walivyobaki navyo baada
ya kuwadhuru wahanga wa matukio hayo ambao wengi wao ni wanawake wenye rika la
wasichana
Kamishna Kova aliongeza kuwa, watuhumiwa hawo
wamekiri kuhusika na mauaji ya WANZE D/O
MAKONGORO, Miaka 23, Mkazi wa Bagamoyo,
aliyekuwa mwanafunzi wa Stashahada ya Ukutubi mwaka wa pili katika Chuo
cha Bagamoyo na JACKLINE D/O FREDERIC MASANJA @ SALHA, Miaka 30 Mkazi wa Kisarawe ambapo wote
waligundulika kuuawa tarehe 19/11/2014 na kutupwa maeneo tofauti ya jiji la Dar
es Salaam.
Vilevile Kamishna Kova alisema Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao
walikutwa na vielelezo ikiwemo Blouses mbili za kike,Sketi moja,Kikoi kimoja,Suriali ya
kike moja,Sidiria moja,Mikoba minne ya kike ,Make-up tatu za kike,Bangili tatu,Shanga
tatu,Kofia ya kulalia ya kike,Vibanio vya nywele na kitana kimoja,Mikufu miwili
pamoja na Hereni pea tatu
Aliongeza kuwa Katika
mahojiano,watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na matukio hayo ya mauaji. Kabla ya
mauaji wamekuwa wakijihusisha na ulaghai wa kimapenzi, utekaji nyara, kuwawekea
dawa katika vinywaji wahanga na hatimaye kuwaibia vitu vyao, kuwanyanyasa
kijinsia na kusababisha mauaji
I kumbukwe kukamatwa kwa watuhumiwa hao imekuja kutokana
na miaka ya hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuripotiwa kuwepo kwa vitendo vya wanawake
hasa wasichana kupata madhara ya kila aina kutokana na wanawake hao kuingia
kirahisi katika mitego ya mapenzi ambayo baadaye hugeuka kuwa madhara
Katika Hatua Nyingeni Jeshi
hilo la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimeendesha
oparesheni iliyoanza tarehe 01/11/2014 hadi tarehe 30/11/2014 ili kuhakikisha
watumiaji wote wa barabara na vyombo vya moto wanazingatia sheria za usalama barabarani.
Oparesheni hiyo imekuwa na mafanikio baada ya kupata Fedha ambazo zinatokana na
Faini Jumla ya Milioni mia sita na
Hamsini na saba elfu laki sita na sitini elfu zimepatikana na Fedha hizo
kupelekwa hazina.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni