HABARI NZITO LEO--UFISADI WA ESROW,TUCTA WAIBUKA WASEMA LIWALO NA LIWE WAMECHOKA SEMA HAPA KUJUA
Pichani ni Rais wa mpya chama cha Wafanyakazi nchi TUCTA Gration Mukoba picha na Maktaba |
Na karoli
Vinsent
CHAMA cha
Wafanya kazi nchini (TUCTA) nao wamejitosa Kwa mara ya Kwanza kwenye sakata la Ufisadi wa
zaidi ya bilioni 400 za kitanzania kwenye Akaunti ya Escrow na kusema chama hicho hakiwezi kukubaliana na ufisadi
huo na kuitaka serikali kuwachukulia hatua kali ya watu wote waliohusika na
wizi.
Na kama endapo Bunge pamoja na serikali hawatawachukulia
hatua zozote Viongozi waliohusika na wizi huo, basi TUCTA itachukua Jukumu la
kuwaunganisha wakulima na wafanyakazi wa idara zote kushikilia bango suala hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar
Es Salaam na Rais Mpya wa Chama
cha Wafanyakazi nchini TUCTA Gration Mukoba wakati wa Mkutano na waandishi wa
habari, ambapo Mukoba alisema wao TUCTA ambao nao pia ni walipa kodi nchini hawawezi
kukubaliana na wizi wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti ya Escrow.
“Kusema
kweli sisi wafanyakazi tumechoka na hali ya Ufisadi unaoendelea nchini, na
ukizingatia sisi TUCTA ni walipa kodi wakubwa sana ,tunasikitika sana kusikia
serikali inaweza kusimamia mambo ya ufisadi yanayotokea maeneo mbalimbali nchini, na sisi vyama vya
Wafanyakazi nchini kwa pamoja tunaiomba serikali iwachukulia hatua kali sana
Viongozi waliohusika kwenye wizi huu wa mali za umma”alisema Mukoba.
Mukoba
aliongeza kuwa kwamba wafanyakazi nchini wanaishi katika mazingira magumu sana
huku wengine bado wakiwa wananchukua mashahara mdogo ambao usioendana na hali
ya maisha ya sasa na wanasikitika kusikia pesa zinaibwa na watendaji wa serikali na huku wakishindwa kuchukuliwa hatua.
Aidha Mukoba aliwashangaa watu ambao
wanasema pesa ambazo zimeibwa kwenye Akaunti ya Escrow kusema sio za umma bali
ni za wamiliki wa Kampuni ya IPTL na
kusema sio kweli kwani pesa hizo ni za
watanzania wote, kwani zimechukuliwa kwenye shirika la Umeme nchini Tanesco.
Vilevile TUCTA wameiitaka Jamii kujiweka
Tayari kuungana nao ili kuchukua maamuzi magumu kuhusu ufisadi huo na kama endapo Serikali itashindwa kuwachukulia
hatua Viongozi waliohusika kwenye wizi huo ambao haujawai kutokea tangu nchi
kupata Uhuru basi wao watachukua maamuzi magumu ambayo Rais huyo akuyataja maamuzi gani.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni