USHINDI WA HALIMA MDEE WA CHADEMA,WAMKUNA RAIS KIKWETE,ASEMA YA MOYONI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
NA Karoli
vinsent
RAIS Jakaya
Kikwete ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM,amekuwa mtu wa kwanza
kwa upande wa Chama chake Kumpongeza,Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Wanawake wa
Chama Cha Demokrasina na Maendeleo CHADEMA BAWACHA,Halima Mdee.
Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe
Chadema,amepewa Pongezi hizo naa Rais Kikwete leo Jijini Dar Es Salaam wakati alipokuwa anafufungua
barabara kati ya mwenge hadi kawe ,ambapo wakati anahutubia wananchi rais
kikwete alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mdee.
“Natumia
Nafasi hii kumpongeza sana Mwanamama Halima Mdee kwa kuchaguliwa kwenye nafasi
ya Umoja wa Wanawake ndani ya Chadema,tena nasikia unataka kuonana na mimi
namwambia karibu tena namngojea”alisema Rais Kikwete
Kwa Upande Halima Mdee mwenye mara baada ya
kupongezwa na Rais Kikwete akusita kutoa lawama zake kwa Viongozi wa mkoa wa
Dar Es Salaam kwa kushindwa kumtaharifu kwake juu ufunguzi wa barabara hiyo na kusema ofis
ya mkuu wa mkuu wa mkoa ilifanya makosa kwani barabara hiyo ipo katika Jimbo
lake.
“Kikweli nasikitika sana yaani wala
sikupewa hata taarifa rasmi juu ya kuzinduliwa barabara hii,licha kusikia kwa
watu,ni jambo lakushangaza sana mimi kama mbunge ninatakiwa nipewa taarifa hili
ni jimbo langu na sijui kwanini viongozi wa mkoa Dar es Salaam wanashindwa
kunipa taarifa ?”alihoji Mdee.
Licha ya Mdee kutoa malalamiko
hayo,Mwandishi wa Mtandao huu alimshudia Mbunge huyo akiende kwenye Jukwaa la wageni Rasmi ambapo ndipo alipokaa
Rais Kikwete huku nafasi yake kutokuwepo na kuwaacha wananchi pamoja na
waandishi wa habari wakishangaa hali hiyo,ila bahati nzuri alipofika jukwaani
kulikuwepo na nafasi moja ambayo hakutakiwa kukaa mbunge huyo lakini yeye
alikwenda na kuketi, kwa maana yake Halima mdee akuwa amepewa mwaliko katika
uzinduzi huo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni