RAIS KIKWETE--NI VIGUMU KUIMALIZA FORENI YA JIJINI LA DAR,ASEMA NI ISHARA YA MAENDELEO SOMA HAPA ZAIDI
PICHANI RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWAHUTUBIA WAKAZI WA TEGETE JIJINI DAR ES SALAAM,WAKATI WA UZINDUZI WA BARABARA KATI YA MWENGE HADI TEGETA |
Na karoli
Vinsent
RAIS Jakaya
Kikwete amesema Tatitizo la Msongamano wa Magari katika Jiji la Dar es Salaam
ni vigumu kumalizika haraka,bali serikali yake inajipanga kuhakikisha
inalipunguza tatizo hilo,
Kwa
kuanzisha usafili wenye haraka kama mradi wa mabasi yaendeyo kwa kasi (DART) ,na
usafili wa reli yaani treni.
Rais Kikwete amesema hayo leo Jijini
Dar Es Salaam wakati wa Uzinduzi wa barabara ya bagamoyo inayoanzia Mwenge hadi
Tegeta,ambapo Rais Kikwete amesema ni vigumu sana tatizo la msongamano wa Mgari
kumalizika kabisa kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaomiliki Magari,
PICHANI NI RAIS KIKWETE KULIA AKIWA NA BAROZI WA JAPANI NCHINI MASAKI OKADA AKIKATA UTEPE IKIASHILIA UZINDUZI RASMI WA BARAARA KATI YA MWENGE HADI KAWE,PICHA NA IKULU |
Na kusema tatizo la msongamano wa
magari katika nchi nyingi Duniani hususani maeneo ya katikati ya Jiji
wameshindwa kuondoa tatizo hilo zaidi ya kuweka usafili utakao wafanya wananchi
wasitumia magari binafsi.
“Kukweli
acha niseme ukweli tatizo la msongamano wa magari katika jiji hili ni vigumu
kuisha,hebu jiulizeni wote tatizo hili lilikuwepo miaka ya nyuma jibu ni hapana
kutokana na kipindi kile watu wenye magari walikuwa wachache tena wakuwahesabu
lakini sasa kila mtu anagari,tena wote wanataka kuja mjini”
HUU NDIO BARAARA ILIVYO SASA |
“Na wakifika katika makutano ya magari
lazima walete foreni tu ndio maana serikali imeona njia raisi ni kuanzisha
usafili wa haraka utakokufanya uacha gari lako nyumbani na utumie usafili wa
haraka na tayari tumeanza kwa kuanzisha usafili wa Mabasi yaendayo kwa kasi na
tuko mbioni sasa kuanzisha usafili wa reli yaani treni”alisema Kikwete
Aidha Rais Kikwete aliitumia nafasi hiyo
kuipongeza serikali ya Japani kwa msaada mkubwa wa kifedha na kitaalamu katika
ujenzi wa Barabara hiyo,ambapo amesema barabara hiyo itawasaidia wananchi wa
jiji la Dar Es Salaam.
Awali akizungumia mradi huo barabara
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi muhandisi Mussa Iyombe amesema Barabara hiyo yenye kilomita 12.9 kutoka mwenge hadi kawe Jijini
hapa ujenzi wake ulianza mwezi februari mwaka 2012 na kazi ya ujenzi rasmi
ujenzi wke ulianza mwezi desema mwaka huo ambapo hadi kukamilika kwake
umeghalimu Bilioni 99.9 za kitanzania ambazo kati ya hizo asilimia 95 ni za
msaada kutoka serikali ya Japani.
Kwa upande wake Barozi wa japani Nchini Masaki
Okanda alisema Serikali ya Japani haitoacha kuisadia serikali ya Tanzania
katika mambo mbalimbali ikiwemo barabara na kuwataka watanzania kuitunza
Miundominu ya Barabara.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni