Zinazobamba

LUDOVICK--CHADEMA ITALETA VITA 2015,AFICHUA MAZITO KUHUSU CHADEMA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

pichani ni Joseph Ludovick picha na Maktaba
Na karoli Vinsent
ALIYEKUWA, mshitakiwa mwenza wa kesi ya ugaidi kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovicki Ameibuka na kusema mazito kuhusu Chadema haya ndio aliyoandika kwenye Mtandao wake

        “Wengi wamekuwa wanaacha kutazama hoja ninazoweka na kukimbilia kunitusi na kunikashfu binafsi. sijali sana hayo kwa sababu naamini natimiza wajibu mkubwa wa kijamii, kukilinda na kukitetea chama changu CHADEMA, na kuilinda nchi yangu TANZANIA. 

         leo natafakari kile ambacho kitatokea baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 kama chama changu hakitabadilika haraka na kuachana na siasa za ki machiaveli. "Makamanda" kama tunavyoitana, tumekuwa ni watu wa mihemuko. hatuhoji chochote hasa kikisemwa na viongozi wetu. 


        Hoja na ushuhuda wangu ni kuwa nafahamu kuwa mara nyingine na hasa juu ya matokeo ya uchaguzi viongozi wetu husema uongo wa hatari, na huko nyuma mimi mwenyewe nimeshiriki kuupika uongo huo. kwa ajili ya hoja yangu, nitatoa mifano mitatu halisi. 

     Wakati wa uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2010 pale Bukoba mjini, tukijua kabisa kuwa tulikuwa tumeshindwa,tuliamua kuwadanganya wapiga kura na hasa vijana waliokuwa wamefurika kwenye kituo cha kujumlisha kura kuwa tumeshinda, wakaanza kushangilia,wakati ukweli tulikuwa tumeshindwa kwa zaidi ya kura 2000, na kwa haki kabisa. 

      Hii ilisababisha vurugu pale wafuasi wa CCM walipoanza kushangilia ushindi halali wa mbunge mteule. Wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga, tukiwa tumejua matokeo kuwa tumeshindwa usiku, na kulingana na upepo tuliokuwa tumewajaza mashabiki wa CHADEMA pale Igunga, tuliamua kuwadanganya wanachama wetu kuwa tumeshinda na tukapita mitaani na gari la matangazo tukishangilia na kukusanya vijana kwenda halmashauri eti kulinda kura zisichakachuliwe. 

      Vijana waliingia mtaani kwa wingi. matokeo yake Matokeo yakasema CCM ndiyo washindi. tulipofika maeneo ya Peak hotel pale igunga wakatokeza vijana wa CCM wakatembeza kipigo cha mbwa mwizi kwa vijana wa CHADEMA. watu walikatwa mapanga na nakumbuka hadi risasi zilifyatuliwa. 

       Mwisho nakumbuka alichosema mgombea wetu baada ya uchaguzi wa rais uliopita. akisema alikuwa ameshinda ila akachakachuliwa. nchi ilikuwa kwenye tension na nadhani vijana wa CHADEMA tulikuwa tayari kuingia barabarani tukiamini kuwa kweli tuliibiwa kura tu uchaguzi wa rais. 

          Hoja yangu ni kuwa kutokana na mazingira ya siasa yalivy sasa,hadi mwaka 2015 kutakuwa na kundi kubwa la vijana bila shaka watakaoweza kuitikia mwito wa viongozi wetu wa CHADEMA kuingia barabarani kama watasema kura zimeibwa ama kujitangaza kushinda wakati wakijua hawakushinda. (maana kushinda urais bado sana), 

     Mapigano makubwa yatatokea baina ya vijana wa chama chetu CHADEMA, na wale wa CCM, na baina yetu na vyombo vya dola. kama CHADEMA itafanya hivi itakuwa imesababisha mauwaji ya raia wasiyo hatia. natamani chama changu kibadilike kabla ya wakati huo. Inawezekana kufanya siasa sakama CHADEMA inavyotarajiwa”

Hakuna maoni