UGOMVI WA POLISI vs JWTZ HUKO TARIME,MAJIBU YAKE HAYA HAPA
Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limelaani kitendo cha askari wake wa
kikosi cha Nyandoto 27 KJ Makoko ambaye inadaiwa alishindwa kutii maelekezo
ya askari polisi wa Usalama Barabarani wilayani Tarime, Mara
na
kusabisha mapigano baina ya wanajeshi na polisi.
Katika
tukio hilo ambalo lilitokea Oktoba Mosi, mwaka huu jioni katika kituo
cha mabasi mjini Tarime, raia mmoja na askari kadhaa wa Jeshi la Polisi
wakiongozwa na Mkuu wa Upelekezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Kanda maalum
ya Tarime /Rorya na askari wawili wa JWTZ walijeruhiwa kwa risasi.
Mkuu
wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya Magharibi, Brigedia Jenerali
Mathew Mayela Sukambi, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi,
alisema kitendo hicho cha aibu kimefanywa na askari binafsi na
siyo
JWTZ.
Alisema
askari huyo amekiuka kiapo chake, hivyo hastahili kuendelea kuitwa
mwanajeshi wa jeshi hilo na kwamba ameagiza sheria na taratibu zichukuliwe
dhidi yake pamoja na wote walioshiriki katika tukio hilo.
“Kitendo
hicho kimefanywa na askari binafsi na siyo jeshi, taratibu za jeshi
zinafundisha na kueleza afisa na askari kuwa mtiifu na mwenye nidhamu
na kutakiwa kutii mamlaka na kufuata sheria za nchi kwa mujibu
wa
katiba,” /ilieleza sehemu ya tamko hilo la JWTZ.
Alisema
kuwa chanzo cha fujo na vurugu hizo zilisabishwa na askari wa Jeshi
la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kumkamata askari wa JWTZ
kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu (Helment) na
baada
ya majibishano askari huyo aliita wenzake waliokuwa jirani kwa ajili
ya msaada ndipo polisi waliitana kwa wingi na kuanza kutumia nguvu
kwa kutumia risasi za moto kuzima vurugu hizo.
Aliwataka
maofisa na askari wa jeshi hilo kuzingatia viapo vyao, kutii sheria
na taratibu za nchi, mamlaka ya kiraia kwa mujibu wa katiba ya Tanzania
huku akiwaonya raia kuacha kushabikia matukio mabaya pindi
yanapotokea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni