HABARI NJEMA-MKONGO WA TAIFA WAKAMILIKA,SASA SERIKALI KUSAMBAZA KWENYE HUDUMA ZA AFYA NCHI NZIMA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
pichani ni Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa |
Na karoli
Vinsent
SERIKALI
nchini imesema ifikapo mwakani mwezi wa kumi Hospitali zote za Rufaa nchini
zitaunganishwa kwenye mkongo wa Taifa kwa lengo la kuboresha huduma za afya
nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar Es
Salaam na Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
akizindua huduma mpya na ya kisasa ya Video ya mikutano,ambapo Profesa Mbarawa
alisema Mkongo wa Taifa umekamilikia kwa asilimia kubwa na kuongeza ifikapo
mwakani watahakikisha hospitali zote nchini zinaunganishwa kwenye mkongo wa
taifa hili kuongeza ubunifu na uwajipikaji kwa watendaji wa Afya.
Profesa Mbarawa alizidi kusema nia
ya Wizara yake ni kuifanya Sekta ya “Internet”Mtandao Inakua kwa kasi hapa
nchini na kuleta Tija katika Taifa huku
ikizingatia Dunia kote sekta ya Mawasiliano imekuwa muhimili wa uchumi
.
Vilevile Profesa Mbarawa alisema kwa
kuzinduliwa kwa Huduma ya Video Mkutanoni itapunguza gharama ilizokuwa
inazipata Serikali kwa kutenga Fedha kwa Watendaji kusafiri kutoka mkoa mmoja hadi mkoa
mwingine kwa ajili ya Kikao lakini kwa mfumo huu mpya uliozinduliwa leo
utawaondolea Adha hiyo na kuwafanya watendaji wa mikoa na Wilaya kukaa walipo
na kutumia njia ya Video kuwasiliana na watendaji wengine pasipo kwenda kwenye
eneo la tukio.
Aidha, Profesa Mbarawa
aliwataka watanzania kutumia mitandao ya Kijamii kwa lengo ya kupata taarifa na
kuongeza ujuzi wa mambo na kuacha tabia hasi ya kutumia mitandao ya Jamii
kuchafua watu na kuonyesha picha chafu.
Huduma ya
Video ya Mkutanoni imeanza kwa Mikoa zaidi ya tano ambapo huduma hiyo
itapunguza urasimu uliopo wa kutumia Fedha nyingi za Serikali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni