SAKATA LA WANAFUNZI KUKOSA MIKOPO-TAHLISO YAZIDI KUIKABA SERIKALI,YATOA MISIMAMO YAO,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Pichani ni Mwenyekiti wa TAHLISO, JUMUIYA ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO(Picha na Maktaba) |
Na Karoli
Vinsent
HUKU ikiwa
bado Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) ikiwa inasuasua kutaja majina ya Wanafunzi
wapya watakaopata Mikopo wa mwaka wa masomo 2014-2015,kutokana na bodi hiyo
kusema inauwezo wa kuwapa mikopo wanafunzi 30000 tu kati ya wanafunzi 58,037 waliomba mwaka huu.
Kwa madai bodi hiyo imepewa Bajeti
ndogo na serikali,Nao Jumuiya ya
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO)imezidi kuibana serikali na
kusema haitokubali kusikia wanafunzi wanakosa mkopo na kusema kila mwanafunzi
wa anayejiunga elimu ya juu nchini anahaki kupata mgawanyo sawa wa keki ya
Taifa
.
Hayo
yamesemwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa
vyuo vya Elimu ya juu (TAHLISO) Musa leonard Mdede, wakati wa
Mkutano na Waandishi na Habari,ambapo alisema maazimio ya Mkutano mkuu wa
Tahliso uliofanyika Chuoni RUCO-Mkoani Iringa,umeitaka Serikali kwamba
wanafunzi wote waliomba mkopo katika mwaka huu wamasomo wapewe wote.
“Mkutano mkuu wa
TAHLISO umeazimia kwamba wanafunzi wote waliomba mkopo mwaka huu yaani
wanafunzi 58,037 wapewe wote kama tu
kutakuwa wamedahiliwa na tume ya vyuo vikuu
kuingia Elimu ya Juu,hili jambo la dharura na tunaitaka serikali
kuhakikisha kufanya hivo kwani wote ni Watanzania wanaostahili mgawanyo sawa wa
Keki ya Taifa”alisema Mdee.
Mdee alizidi
kusema Jumuiya hiyo imeitaka Bodi ya Mkopo kuacha kutoa Mkopo kwa ubaguzi
kutokana na hivi sasa kutoa upendeleo kwa watu wenye kada ya masomo ya Sayansi
na Elimu na kuzipa kisogo Taaluma nyingine kwani bodi kufanya hivyo kutalepelekea Taifa
likose wasomi katika masuala mengine ikiwemo Uandishi wa habari,mambo ya Fedha
na sheria.
Vilevile
Jumuiya imeitaka serikali kupandisha kupandisha mara moja fedha ya kujikimu kwa
mwanafunzi wa elimu ya juu toka 7500/kwa siku hadi 15000 na kusema hali ya
maisha imependa huku ikizingatiwa garama za vitu viko juu tofautisha na kipindi
kile cha nyuma walipopitisha kiasi hicho.
Aidha Mdee aliitaka Tume ya Vyuo Vikuu
nchini TCU kusimamia misimamo yake ya mwanzo ambayo ilikuwa inavitaka vyuo
Vikuu vyote nchini kutopandisha Ada ya Masomo kutokana na hivi sasa vyuo vya
KCMC na St Francis kilichopo Ifakara ambapo vyuo hivyo vimekaidi walaka wa tume
ya vyuo vikuu nchini iliyovita vyuo
visipandishe ada za masomo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni