MASIKINI WALIOBA-- SASA CHADEMA WAMKARIBISHA RASMI KAMBINI
MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA), Halima Mdee,
amewakaribisha katika chama hicho, wajumbe wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji mstaafu Joseph Warioba, akisema
wanawathamini kama wafalme kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Mdee alitoa ukaribisho huo juzi wakati akizungumza na umati mkubwa
wa wananchi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye uwanja wa
Getrude Mongela mjini Nansio, wilayani Ukerewe.
Alisema kuwa Warioba na wazee wenzake kwenye tume yake, wamelitumikia
Taifa kwa uadilifu mkubwa bila kukwapua fedha za Umma, na kwamba
walifanya kitendo cha uadilifu mkubwa cha kuweka kando maslahi ya vyama
vyao ili kuhakikisha maoni ya wananchi zanazingatiwa kwenye rasimu.
“CHADEMA na UKAWA tunawatamani kweli, kama chama chao hakiwapendi na
wao hawataki kuhama, wakifukuzwa yaani kwetu watapokelewa kama wafalme…
karibuni sana,” alisema Mdee huku akishangiliwa.
Kuhusu katiba mpya inayopendekezwa, Mdee alisema kuwa muungano wa
wanawake wanaharakati wa Katiba, umewasaliti wanawake nchini kwa tamko
la kwamba katiba hiyo imezigatia maslahi ya wanawake kupata haki zao.
Mdee alisema kuwa miongoni mwa wanawaharakati waliotoa tamko hilo
ni wanawake aliokuwa akiwaheshimu toka akiwa mdogo akiamini kuwa
ni watetezi wa wanawake lakini kwa kitendo chao cha kushindwa
kusimamia maslahi ya wanawake wenzao, kimemsikitisha sana.
Akiwa ameambatana na Makamu Mwenyekiti, Hawa Mwaifunga, Katibu Mkuu,
Grace Tendega, Naibu Katibu, Kunti Yusuph na Katibu Uenezi wa
BAVICHA, Edward Simbeye, Mdee alisema kuwa hoja ya uwakishi sawa 50 /50
kwenye nafasi za uongozi si kipaumbele cha wanawake wa Tanzania.
Alisema kuwa wanachotaka ni katiba kuhakisha upatikanaji wa huduma
muhimu ikiwemo afya, elimu bora kwa watoto wao na fursa za kiuchumi kuwa
ni haki yao kikatiba.
“Wanasema kuwa wanaipongeza katiba pendekezwa kwa kutoa fursa ya 50
/50 kwenye nafasi za uongozi, hivi kweli hiki ni kipaumbele cha
wanawake?
Kuhusu katiba mpya inayopendekezwa, Mdee alisema kuwa muungano wa
wanawake wanaharakati wa Katiba, umewasaliti wanawake nchini kwa tamko
la kwamba katiba hiyo imezigatia maslahi ya wanawake kupata haki zao.
Inamsaidiaje mwanamke wa kijijini. Wanawake wanataka
katiba iwahakikishie upatikanaji ya huduma muhimu na fursa muhimu
na wakizikosa waweze kwenda kuzidai mahakamani,” alisema.
Naibu Katibu wa BAWACHA, Kunti Yusuh, aliwataka wanawake wa CCM
kuacha kujiita wao ni Umoja Wanawake wa Tanzania (UWT) kwa kile
alichodai si wanawake wote wa Tanzania wako kwenye chama hicho.
“Wameshindwa kutuletea huduma bora za afya, wameshindwa
kutuhakikishia elimu bora kwa watoto wetu, katiba haituelezi vipi
tutadai haki ya kupewa fursa zetu kiuchumi, wanatuambia tutapewa nafasi
50/ 50 kwenye uongozi, nani kasema hiki ni kiaumbele cha wanawake?
Alihoji.
Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli (CHADEMA), alisema kuwa kwenye
jimbo hilo hakuna mzazi atakayechangishwa mchango wa ujenzi wa maabara
kama ilivyoagizwa na Rais.
Alisema kuwa maabara hizo zitajengwa na halmashauri ya wilaya kwa fedha za kodi inayokusanywa kutoka kwa wananchi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni