INASIKITISHA-HIVI NDIVYO SAMWEL SITTA ALIVYOCHAKACHUA KURA ZA WAJUMBE UPANDE WA ZANZIBAR,ILI KUIPITISHA KATIBA YA CCM.SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na karoli
Vinsent
MCHEZO mchafu uliofanywa na Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta wakati wa kupata seluthi
mbili kwa upande wa Zanzibar ili kupitisha Rasimu ya Katiba ya Chama cha
Mpinduzi Imefichuka Mtandao huu umebaini.
Habari za
kuaminika ambazo Mtandao huu umizipata kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa CCM,
zinasema kuwa akidi inayotakiwa kutoka Zanzibar kupitisha Katiba
inayopendekezwa, ilikwama lakini ilibidi kura zichakachuliwe kukidhi matakwa ya
kisheria.
Mtandao hu
umebaini Mchanganuo wa kura halisi uko hivi; Wabunge wote wa Bunge Maalum la
Katiba, wako 629 kati yao 419 wanatoka Tanganyika na 210 wanatoka Zanzibar.
Wajumbe
wanaotoka Zanzibar wako 210 na theluthi mbili yao ni 140. Wajumbe wa UKAWA
kutoka Zanzibar waliotoka bungeni, wako 67 na wajumbe kutoka Zanzibar waliopiga
kura ya hapana wako wanane.
Na ili kuinyima
Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa isipite, kura 71 ambayo ni theluthi mbili
(2/3) ya Zanzibar ilitosha kabisa kukwamisha mchakato huo.
Hivyo wajumbe 67
wa UKAWA wakijumuishwa na wajumbe saba waliosema ‘Hapana’, wanapatikana 75
hivyo waliopitisha katiba inayopendekezwa ni chini ya 135.
Mtandao huu pia
umebaini, Idadi ya wajumbe wa UKAWA, ukiongeza kura mbili, moja ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Abdallah Abas na Othamn Masoud, kisha kuchanganya
za wale wajumbe waliopiga kura ya Hapana, jibu liko wazi akidi haikutimia.
Vilevile UKAWA
walihitaji kura 71 tu kuzuia Katiba ya Mpya, wajumbe 67 ukiongeza na wajumbe
wawili, Othamn Masoud na Abas, idadi ya wajumbe inafikia 69 na ukiongeza kura
zilizosema ‘Hapana’, akidi ya Zanzibar haitatosha.
Hesabu hizo ni
bila kuzingatia matokeo ya kura zilizopigwa kwa siri na waliopiga kura wakiwa
nje ya Bunge Maalum.
Mtandao huu
ukadokezwa Hata kama kura zote zingekuwa zimeikubali katiba inayopendekezwa
zisingeweza kubadilisha uhalisi na ukweli wa kitakwimu za kukosekana kwa akidi.
Kwa uchunguzi wa uliofanywa na Vyanzo mbalimbali unasema theluthi mbili ya kura za wajumbe wote wa
Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar haikuwapo na kilichofanyika ni uchakachuaji
ili kupisha katiba iliyojaa mapendekezo ya ccm.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni