HAKI ZA BINADAMU KUCHUNGUZA UCHAKACHUAJI WA THELUSI 2 ULIOFANYWA NA SAMWEL SITTA,ZAIDI SOMA HAPA KUJUA
Pichani Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk Helen Kijo Bisimba picha na Maktaba |
MKURUGE NZI wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, amesema watafanya uchunguzi
kubaini mazingira yaliyowezesha kupatikana kwa theluthi mbili ya wajumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar.
Alisema ingawa Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa imepitishwa, theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar haijulikani
inatokana na kura gani, kwani toka awali hesabu zilionyesha kura za wajumbe
kutoka visiwani zisingefikisha idadi inayotakiwa.
“Pamoja na kupitishwa hiyo rasimu,
bado kuna utata wamepataje theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar,
tutafuatilia tujue imetokea wapi, kwa hesabu tulizokuwa tunapiga kulikuwa
hakuna uwezekano,” alisema Dk. Bisimba.
Aidha alisema hata hivyo bado
wananchi wana nafasi ya kuchuja katika kura ya maoni kuangalia ni mambo yapi
waliyatolea maoni waliyotoa yapo katika Rasimu ya Katiba hiyo inayopendekezwa
na yapi yametolewa, na ndipo wafanye uamuzi.
“Wananchi waelewe kuwa kupitishwa
kwa rasimu ya tatu si mwisho wa mchakato, bali tunawasubiri katika kura ya
maoni,” alisema.
CHANZO NI MTANZANIA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni