RAIS KIKWETE AKUMBUKA SHUKA ASUBUHI,SASA AANZA KUMCH0KA WAZIRI NYALANDU MDA WOWOTE ATACHUKUA MAAMUZI MAGUMU,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Rais Jakaya Kikwete |
RAIS Jakaya
Kikwete ameanza kuchoshwa na vituko vya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu, Chanzo chetu kimethibitishiwa.
Habari za
uhakika zinasema Rais Jakaya Kikwete sasa hana mpango mwingine isipokuwa
kuchukua ‘uamuzi mgumu’ dhidi ya waziri huyo, anayekabiliwa na kashfa nyingi.
Miongoni mwa mambo ambayo rais
anatajwa kukasirishwa nayo ni kitendo cha Nyaladu kutelekeza wizara pamoja na
vikao vya Bunge Maalum la Katiba; na badala yake kuhamishia shughuli zake
jijini Arusha, Marekani na Ulaya.
Pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazro Nyalandu picha na Maktaba |
Nyalandu amekuwa akisafiri ndani na
nje ya nchi huku gharama zote zikibebwa na taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii. Ana vyumba maalum katika hoteli kadhaa za kitalii kwenye
majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Inaelezwa kwamba imekuwa nadra mno
kuonekana ofisini kwake Dar es Salaam; na hata anapotaka kuzungumza na
waandishi wa habari, amekuwa akitumia hoteli za kitalii kwa gharama kubwa.
Chanzo cha
habari kutoka kwenye msafara wa Rais Kikwete nchini Marekani, kimesema kiongozi
huyo mkuu amekasirishwa na hatua ya Nyalandu kwenda nchini humo 'kinyemela' na
kuendelea na shughuli zisizokuwa kwenye ratiba ya rais.
Katika ziara hiyo, Nyalandu
anatajwa kwenda na mmoja wa wasanii waBongo
Movie anayetajwa kuwa
rafiki yake wa karibu.
“Rais yupo
Marekani, kukawa na shughuli inayohusu ujangili na utalii. Mshauri mmoja
akapendekeza Nyalandu awepo ajibu hoja; ndipo Rais aliposhtuka na kuhoji iweje
waziri huyo awe Marekani wakati wenzake wanapambana bungeni kupitisha Rasimu ya
Katiba.
“Lakini rais alionesha
kutofurahishwa na Nyalandu anavyoiacha ofisi pamoja na mparaganyiko mkubwa wa
kiuongozi ulioikumba Wizara ya Maliasili na Utalii,” kimesema chanzo chetu.
Hasira za
rais zinatajwa kumfanya Nyalandu afunge safari haraka ya kurejea nchini
mwishoni mwa wiki iliyopita. Lakini chanzo chetu cha habari kinasema Nyalandu
amekuwa hana wasiwasi wowote wa kupoteza nafasi yake kutokana na kujiamini kwake
kuwa yuko karibu mno na baadhi ya mawaziri waandamizi pamoja na Rais Kikwete
mwenyewe.
Wakati hayo yakitajwa upande wa Rais
Kikwete, kuna habari zisizotiliwa shaka kuwa wabunge kadhaa kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na wengine kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wanajiandaa
kuibana mamlaka ya uteuzi kuhakikisha Nyalandu anang’olewa.
“Haiwezekani kashfa zote hizi zikawa
zinaandikwa, hazikanushwi na bado huyu mtu anaendelea kuwa waziri. Tunasubiri
Bunge la Novemba tuibane mamlaka ya uteuzi imuondoe. Huyu mtu hafai kuwa
waziri. Tunataka tujue hiki kiburi anakitoa wapi?” amesema mmoja wa wabunge
aliyesema ameanza kuandaa hoja ya kumng'oa waziri huyo.
Pamoja na Nyalandu, Naibu wake,
Mahamoud Mgimwa, naye yuko kwenye hatihati kutokana na kukumbwa na kashfa ya
ugawaji vitalu vya miti.
Kwa siku
kadhaa sasa, vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kashfa hiyo, huku Mgimwa
akitajwa kuwa miongoni mwa wahusika wakuu ambao, ama wamejichotea, au
wamefanikisha kuwasaidia marafiki zao kujipatia vibali vya ukataji miti kwa
ajili ya mbao.
Kwa Nyalandu, idadi ya kashfa
zinazomkabili ni kubwa mno. Kashfa ya karibuni ni mpango wake wa kuigomea Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma iliyoamuru kuhamishwa kwa baadhi ya
watumishi wa Maliasili na Utalii.
Waziri huyo aliandika dokezo
akiwazuia watumishi hao, akiwamo Paulo Sarakikya, kwenda walikopangiwa. Hadi
wiki iliyopita, Sarakikya hakuwapo katika kituo chake kipya cha kazi.
Bado
wachunguzi wa mambo wanashindwa kubaini nguzo inayompa jeuri Nyalandu, lakini
kuna habari kwamba wanapata nguvu kubwa kutoka kwa mawaziri wawili wanaotajwa
kuwania urais.
Kashfa
nyingine inayomtikisa Nyalandu ni ya kutoa Leseni ya Rais kuua wanyampori 704;
‘zawadi’ ambayo aliwapa marafiki zake Wamarekani wa familia moja.
Chanzo hicho
kililifanya kazi
kubwa ya kuandika habari hizo na hivyo kufanikisha kuokoa wanyama hao 700.
Pamoja na
habari hiyo, Chanzo kilichapisha picha zilizowaonesha
watoto wadogo wakiwa na bunduki wakiwinda katika kitalu kinachomilikiwa
kihalali na kampuni ya Green Miles Safaris (GMS). Kifungu cha 43(3) cha Sheria
ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009 kinazuia watoto chini ya miaka 18 kuwinda.
Waziri Nyalandu amekiuka kifungu
kinachoweka ukomo wa idadi ya vitalu ambao ni vitalu vitano kwa kampuni.
Ameruhusu TGTS kumilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi na hivyo
kukiuka kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009.
Kwa kawaida
kitalu chochote kinapobaki wazi, sharti kitangazwe kwanza na waombaji
washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya
Uwindaji wa Kitalii 18(1)]. Pia amevunja sheria hiyo kwa kuruhusu uwindaji wa
kitalii kufanyika eneo la Makao, sehemu ambayo haijatengwa kama kitalu.
Kashfa nyingine kwa Nyalandu ni
mpango wake wa kusafiri kwenda nchini Afrika Kusini na kufanya mazungumzo
na kampuni ya African Parks Network (APN) kwa ajili ya kuikabidhi uendeshaji wa
Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu.
Kwenye
mpango huo, alishirikiana na mmoja wa wakurugenzi katika Bodi ya APN, ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii,
James Lembeli.
Kwa mara
nyingine,
Chanzo ililifichua kashfa hiyo na kwa sasa
bado wanatafuta mbinu nyingine za kuuendeleza.
Kwenye
mlolongo wa kashfa hizo, Nyalandu alikuwa na mpango wa kufungua mpaka wa
Bologonja unaotenganisha Tanzania na Kenya ili kuruhusu watalii kutoka Kenya
kupita eneo hilo. Mpaka huo ulifungwa wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya Taifa.
Kwa mara nyingine, Chanzi
hicho kilifichua
mpango huo na kuchapisha nyaraka mbalimbali na hatimaye kufanikiwa kuuzima.
Waziri
Nyalandu anakabiliwa na kashfa ya kujihusisha na ujangili mkoani Singida.
Nyaraka ambazo Chanzo hicho inazo zinaonesha kuwa Juni 11, 2012
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwanyonye, Rehema Manji, alimwandikia Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida akilalamikia kutishiwa kwa bastola.
Anasema, “Napenda kutoa taarifa ya
kuvunjiwa geti/kizuizi cha mazao na kutishiwa kwa silaha aina ya bastola na mtu
ndani ya gari Na. T505 BKM usiku wa kuamkia leo tarehe 11/04/2012 yaani saa
6.00 usiku katika eneo la Kijiji cha Mwanyonye na Kinyeto.”
Aliongeza;
“Pia tumefungua kesi Na. IR/SI/1570/2012, aidha tangu usiku huo hadi sasa geti
liko wazi na magari ya mizigo yanapita bila kukatiwa risiti za ushuru.”
Siku hiyo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya Singida alipokea waraka wa Meneja wa Mkoa wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida, ukisema; “Nakiri kupokea barua yako
ya tarehe 11/04/2012 yenye kumb.SDC/K.2/1/PART ‘E’/45 kuhusiana na somo tajwa
hapo juu. Napenda kukufahamisha kwamba mmiliki wa gari Na. T505 BKM ni Ndugu Lazaro
Samwel Nyalandu mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN: 105-059-701).”
Barua hiyo
ilitiwa saini na Mnubi kwa niaba ya Meneja wa Mkoa wa TRA Mkoa wa Singida.
Pamoja na tuhuma hizo za ujangili, rekodi hazioneshi kama Nyalandu alishawahi
kuwajibishwa kwa jambo hilo.
Chanzo ni
Gazeti la Jamhuri
Hakuna maoni
Chapisha Maoni