Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO-SAMSONI MWIGAMBA ALIPUKA,AWAMWAGIA SIFA UKAWA KUUNGANA,NA ASEMA MENGI KUHUSU CHAMA KIPYA CHA ACT,SOMA HAPA KUYAJUA


Katibu mkuu wa chama cha ACT TANZANIA--SAMSON MWIGAMBA akizungumza na
waandishi wa habari ofisi za chama hicho kijitonyama jijini dar es
salaam muda huu kuhusu mambo mbalimbali katika chama hicho


Exaudi Mtei na Karoli Vinsent
Ikiwa imepita siku moja tangu umoja wa katiba ya wananchi UKAWA
kusaini makubaliano ya kuunganisha vyama vyao kwa lengo la kuwa na
nguvu zaidi ya kisiasa katika chaguzi zijazo nacho chama kipya katika
siasa za Tanzania cha ACT-TANZANIA  kimeibuka na kupongeza hatua hiyo
na kuunga mkono harakati hizo za kisiasa za kuunganisha nguvu ya
upinzani kwa kusema kuwa kufanya hivyo itawasaidia kukiangusha chama
cha mapinduzi kirahisi huku akitoa tahadhari kwa muungano huo.

 Akizungumza na wanahabari muda huu katika ofisi za chama hicho kuhusu
maadhimio ya mkutano wa kamati kuu ya chama hicho katibu mkuu wa ACT
Samson mwigamba pamoja na kutokuweka wazi kuwa chama chake kipo tayari
kujiunga na UKAWA amesema kuwa ni hatua nzuri kwa siasa za upinzani
kama muungano huo utakuwa ni muungano wa sera na kutetea wananchi huku
akisema chama chake kitaungana na chama ambacho kipo tayari kuwatetea
wanachi na sio kwa ajili ya kuiangusha CCM ili wagawane madaraka ya
serikali.

“Muungano wa ukawa ni hatua nzuri katika siasa  ila tunatoa tahadhari
sana kwa muungano huo usije ukawa ni muungano wa kugawana madaraka,
sisi tutaungana na yeyote ambaye yupo tayari kuwatetea wananchi ila
hatutaungana na watu ambao watakuwa wanataka kuiangusha CCM ili
kuingia ikulu na kugawana madaraka”Amesema MWIGAMBA.


Aidha akizungumzia katiba iliyopendekezwa katibu mkuu huyo amesisitiza
kile ambacho na UKAWA walisisitiza kwa kusema kuwa katiba
iliyopendelezwa ni wizi na udanganyifu mkubwa kwa wananchi ambao
umefanywa na chama cha mapinduzi hivyo nao wanatangaza rasmi kuzunguka
nchi nzima kuwahamasisha wananchi wote kupiga kura ya hapana kwa
katiba iliyopendekezwa kwa kile walichodai kuwa haijakidhi mahitaji
nya watanzania kwa sasa.

“Chama cha ACT kwa nia moja tumeamua kuzunguka kwa watanzania wote
kuhamasisha kura ya hapana kwa watanzania na zoezi hilo litaanza mara
moja kwa kuwa katiba hii iliyopendekezwa haijakidhi matarajio  na
maoni ya watanzania wote.

Akikizungumzia cha hicho kipya amesema kuwa ACT kitazinduliwa rasmi
tarehe 5 december mwaka huu jijini Dare s salaam ambapo kwa mujibu wa
katiba ya chama hicho kutafwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara wa
uzinduzi wa chama hicho ambao utafanyika jijini mwanza.

Hakuna maoni