TIBAIJUKA ASISITIZA USHIRIKIANO DUNIANI KUKABILI CHANGAMOTO MBALIMBALI
Baadhi ya wakuu wa mashirika
mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakiwapokea wageni waalikwa kwenye
hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa
iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Na Mwandishi wetu
Tanzania imetaka jumuiya za
kimataifa na washirika wa maendeleo kuhakikisha wanashirikiana na Umoja
wa Mataifa kuhakikisha kwamba madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa
Mataifa (UN) yanafikiwa.
Umoja wa Mataifa ulianzishwa miaka
69 iliyopita kuhakikisha amani, maendeleo na ukuaji wa demokrasia ili
kuifanya dunia hii kuwa mahali bora pa kuishi.
Kauli ya Tanzania imetolewa
kupitia Waziri wake wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka mwishoni mwa wiki wakati wa kilele cha sherehe za miaka 69 ya
Umoja wa Umoja.
Alisema hayo katika hafla ya mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya UN iliyofanyika jijini dar es salaam.
Alisema jukumu la Umoja wa Mataifa
la kuwezesha maisha bora duniani haliwezi kufanikiwa kama kusipokuwapo
ushirikiano wa dhati wa kukomesha changamoto zinazokabili dunia hii kama
umaskini uliokithiri, ugaidi na magonjwa.
Alisema kwa miongo mitatu Umoja wa
Mataifa umejituma katika kutekeleza wajibu wake hasa katika kuleta
usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira, kuelekeza maendeleo ya pamoja na
kuhakikisha amani inapatikana.
Alisema mikutano mbalimbali ya
kimataifa iliyofanyika kama ile ya Stockholm, Vancuva, Beijing ililenga
kuweka msimamo wa pamoja ambao unawezesha dunia kuwa mahali pa amani
ambapo mataifa yanashirikiana kuiweka salama dunia, kwa kuangalia
changamoto za demokrasia,mabadiliko ya hali ya hewa na usawa wa binadamu
huku suala la wanawake na watoto likitiliwa maanani.
Alisema juhudi za Umoja wa Mataifa
umewezesha mabadiliko makubwa kuwepo ambapo dunia kama moja inafanya
juhudi za kuimarisha ushiriki wa wanawake katika maendeleo, kuwa na
sauti moja katika kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwemo vita na
magonjwa.
Hata hivyo alisema pamoja na
mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali za afya, amani na
maendeleo na kuleta usawa wa jinsia na kushughulikia afya na maendeleo
ya wanawake na demokrasia, bado UN ina changamoto kubwa inayoambatana na
maendeleo yaliyopo.
Alisema umaskini uliokithiri na
ugaidi umekuwa chanzo kipya cha migogoro inayotishia amani na maendeleo
ya dunia. Alizitaka nchi wanachama kuungana kuhakikisha kwamba
changamoto hizo zinatokomezwa.
Akimkaribisha Waziri Tibaijuka
kuongea Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez, alisema kwamba wamefurahishwa na hatua iliyofikiwa na
Tanzania katika kutekeleza malengo ya milenia na kwamba Umoja wa Mataifa
utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kwamba malengo
yale ambayo hayakufikiwa yanafanyiwa kazi katika mpango wa maendeleo
ujao.
Aidha alishukuru Tanzania kwa kuipatia UN eneo la kujenga makazi kwa ajili ya mashirika yake yanayofanyakazi nchini .
Pia alisema kwamba wakati Umoja wa
Mataifa unajikita katika kufanikisha maisha bora kwa wakazi wa duniani,
inatambua changamoto zake zilizopo sasa ambapo mamilioni ya wananchi
wanateseka kwa kunyonywa, usafirishaji haramu wa watu na kufanyishwa
utumwa wa kingono.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke wakati wa zoezi la
kupokea wageni kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja
wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Alisema ili kuwa na maendeleo na
haki ni lengo la Umoja wa Mataifa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma
katika maendeleo ya kubadili dunia kuwa mahali bora pa kuishi.
Alisema wakati mpango wa malengo
ya milenia unaisha mwakani ni vyema mataifa yakaendelea kufikiria
kutekeleza yale ambayo haya kuwezekana katika agenda zao za maendeleo.
Alisema amefurahishwa na kauli ya
serikali ya Tanzania kwamba imejipanga kuhakikisha inadhibiti ugonjwa wa
Ebola na pia kuandaa mipango kwa vijana kupata ajira na kukabili
mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha katika hotuba yake amesema
kwamba kwa kuzingatia kwamba nguvu kazi kubwa sasa ni vijana ni vyema
jamii ikaacha vijana waongoze kwa kuwa wao ndio wazazi wa kesho na pia
ndio nguvu inayotakiwa katika ubunifu na uendeshaji wa shughuli za
maendeleo.
Aidha alisema jumuiya ya kimataifa
ni lazima itambue ushirikiano kama njia pekee ya kukabiliana na
changamoto za dunia kwani hakuna nchi moja inayoweza kufanya shughuli
yoyote peke yake.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka wakati wa zoezi la
kukaribisha wageni kwenye hafla mchapalo ya maadhimisho ya miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushi akiteta jambo na baadhi ya wageni
waalikwa akiwemo Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker
(waliyeshikana mkono) kwenye hafla mchapalo iliyoandaliwa na Umoja wa
Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 69 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi ,
Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa FAO, Diana Templeman mara baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na
maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akiwasili kwenye hafla
mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika
mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha
hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuanzishwa kwake.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, mgeni rasmi Waziri wa Ardhi ,
Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri wakati hafla hiyo ikiendelea.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Tibaijuka kuzungumza na wageni waalikwa
kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi,
Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala
yake kwenye hafla hiyo ambapo alitoa pongezi kwa Umoja wa Mataifa kwa
niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea
kushirikiana bega kwa bega na Umoja huo kuhakikisha malengo ya milenia
yanafikiwa kwa asilimia mia moja.
Profesa Tibaijuka na Bw. Rodriguez wakijiandaa kufanya “cheers” ya kuutakia kheri Umoja huo.
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi,
Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mratibu Mkazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakigonganisha glass
“Cheers” kuutakia kheri Umoja huo kwa kutimiza miaka 69.
Pichani juu na chini baadhi ya
wageni waalikwa wakiwamo mabalozi na wadau wa taasisi mbalimba za
serikali na zisizoza kiserikali waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika
jijini Dar mwishoni mwa juma.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni