Zinazobamba

HABARI NJEMA TOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI HII HAPA, SASA MIKOPO NJENJE

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati), akikagua jengo la Mahakama ya Mafunzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu wake, Angellah Jasmine Kairuki na kulia ni Mkuu wa taasisi hiyo, Jaji Dk. Gerald Ndika.

Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria ya mikopo itakayosimamia mikopo kwa wanafunzi  wa vyuo vikuu nchini kikiwamo Chuo cha Sheria Tanzania (IJA), ili kupanua fursa za masomo kwa Watanzania.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea majengo ya Ija Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro,  alisema muswada wa sheria hiyo unatarajiwa kupitishwa rasmi Bungeni Novemba mwaka huu.

Alisema katika bajeti ya serikali Ija hakikuwa katika orodha ya mikopo endelevu kama vinavyopewa vyuo vingine, hivyo maboresho ya sheria hiyo yatalenga muendelezo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wote kwani baadhi yao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na rasilimali fedha.

Alisema mchakato wa kubadilisha sheria utakamilika rasmi 2016, baada ya serikali kukamilisha taratibu zake, na itawasaidia kundokana na misukosuko waliyokuwa wakiipitia wanavyuo wa awali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ija, George Masaju, alisema changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini ni rasilimali fedha kupitia  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya  Juu (HELSB).

Hali hiyo imetafsiriwa na wadau wa elimu kuwa itapanua wigo wa wanafunzi wanaohaha kupata mikopo lakini wamekuwa wakishindwa kupata mikopo kwa wakati.

Hakuna maoni