UKARABATI WA DHARULA KUFANYIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME, MRADI KUGHARIMU FEDHA ZA KINORWAY MILLION 67.5
Katika kuboresha huduma zake za kutoa umeme wa uhakika kwa watanznia, shirika la umeme hapa nchini Tanesco linatarajia kufanya ukarabati mkubwa wa mitambo yake katika vituo vyake vyote vya kuzalisha umeme na kwa kuanzania wameanza na ukarabadi wa dharul;a utakaohusihs vituo vyote vya kuzalisha umeme,
Akizungumza na waandishi wa habari hapa nchini, Naibu mkurugenzi wa uzalishaji wa shirika hilo hapa nchini, Cng. Boniface S. Njombe amekiri kuwepo kwa mradi huo wa dharula wa kukarabati hali ya vituo vya kuzalisha umeme hapa nchini, mradi ambao unaidawa kughalimu kiasi cha shilingi millioni 67.5 fedha za Kinorway,
Eng. Njombe ameendelea kusema kuwa mradi wa ukarabati wa dharula wa hali ya vituo vya kuzalisha umeme tayari uko katika hatua nzuri, na kwamba tayari makarasi washapatikana wa kufanya kazi hiyo ya ukarabati wa vituo hivyo,
WAKANDARASI WATAKAOFANYA SHUGHULI YA UKARABATI. |
Ametaja vituo ambavyo vitanufaika na ukarabati huo wa dharula kuwa ni pamoja na kituo cha Kihansi, Kidatu,Nyumba ya mungu, na Mtera ambayo amedai ikikamilika kutasaidia sana kuongeza ufanisi wa kuwahudumia watanzania kwa wakati na huduma ya uhakika,
Amesema, hatua ya kufanya ukarabati wa dharula umekuja kufuatia tafiti zilizofanywa hivi karibuni na kuonyesha kuwa kuna baadhi ya kzi zinahitaji ukarabati wa dharula (Emergency Repair) hivyo wameamua kuanza na matengenezo hayo kabla ya kuja na matengenezo ya kina hapo baadae
source Tanesco
Hakuna maoni
Chapisha Maoni