NCHI YAZIDI KUTEKETEA KWA UFISADI,SOMA KWA MAKINI UONE JINSI BANDARI INAVYOMALIZWA
Na Karoli Vinsent
WAZIRI wa
Uchukuzi Dk Harison Mwakyembe Ameingia kwenye Kasfa Nzito ,kutokana na Kitendo
chake cha kushindwa kumchukulia hatua,
Kaimu
mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),Mzee Maden
Kipande,ambaye ameguza Mamlaka hiyo kuwa Genge la Ufisadi.
Dk
Mwakyembe,ambaye anasifika kwa Wananchi kutokana Uchapakazi wake na kutokuwa na Nidhamu ya
Uwoga asiyemwogopa mtu yeyote ,ambae atakuwa anavunja Sheria za Nchi alikuwa anamwajibisha.
Lakini,mambo
yamebadilika kwa Waziri hiyo,ambapo sasa ameonekana ameshindwa kumchukulia hatua,Kaimu
mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari
Kipande,kutokana na Vitendo vyake vya kifisadi.
Kwa Mujibu
wa vyanzo vya kuaminika kutoka katika
Mamlaka hiyo ambayo ni kitovu cha Maendeleo ya Nchi yetu ambazo mwandishi wa mtandao
huu amezipata ,zinasema mkurugenzi huyo amekuwa akiwasimamisha wafanyakazi
kinyume na Taratibu na sheria.
Chanzo hicho
kinasema mkurugenzi huyo,amekuwa akiwasimamisha watu tu pasipo kuwa na kosa
lolote kwa mfano mwishoni mwa mwezi uliopita ameanzisha Mpango wa kumngoa
Meneja wa Bandari ya Tanga,Hassani Kyomile eti akisema Meneja huyo amekuwa
akivujisha siri kwenye Gazeti moja la wiki akidai Mhariri wa Gazeti hilo ni Mhaya ,na
meneja huyo pia ni mhaya eti anavujisha siri kwenye Gazeti hilo,ambapo kipande
anaona kumfukuza meneja huyo kutarahisisha mipango yake ya kifisadi pasipo
kuvuja.
Chanzo hicho
kilizidi kusema Kipande amekuwa
akijivunia kwa Wanyakazi wake kwamba anaweza kufanya lolote na hakuna wakumzuia,ambapo
amesimamisha watu kazi zaidi ya miaka miwili huku wakiwa wakipokea mishahara pamoja na
malupulupu huku wakiwa nyumbani bila hata ya kufanya kazi.
Chanzo hicho
kiliwataja wafanya kazi hao,miongoni mwao ni Mama Muhindi,ambaye alikuwa
Mkurugenzi wa Masoko TPA,ambaye alisimamishwa kazi na Kipande kwa Madai alikuwa
anavujisha siri(madudu)za TPA kuhusu
kwenye vyombo vya Habari,licha ya mkurugenzi kipande alishindwa kutokea
wala kukanusha kwenye vyombo vya Habari juu ya Ufisadi huo ,
Tuhuma,zinginene
zinazozidi kumkabili kipande kuhatarisha
usalama wa Bandarini kwa kutokuna na kutokuwepo na Kamera CCTV pamoja na
mita za kupima mafuta yanayoingia nchini kutokafanya kazi kwa miaka mitatu
sasa.
Jambo la
kushangaza Mama huyo Muhindi,alisimaishwa kazi tangu agosti 2013 na
kipande,lakini hajahojiwa wala
kurudishwa kazini ,huku akizidi kuendelea kuchukua mshahara na Marupumarupu
mengine bila kufanya kazi hadi sasa wala hajahojiwa na mamlaka yeyote.
Chanzo,hicho
kilizidi kutaja orodha ya Wafanyakazi
walionewa na Kipande ambae ni Mfanyakazi
mwingine ndugu Msemo,aliyekuwa Afisa Ununuzi,naye alisimamishwa kazi
tangu agosti2013 kwa tuhuma zisizokuwa za Ukweli wowote, lakini mpaka sasa naye
anaendelea kuchukua mshahara pamoja na marupurupu yote pasipo kufanya kazi.
Waliosimamishwa
na kipande kwa tuhuma hewa
Hery
Arika,aliyekuwa Men eja Biashara wa Bandari ya Dar es Salaam,alihamishiwa makao
makuu na kuambiwa kuripoti idara ya utawala tangu April 2013 hadi leo
hii,Analipwa mishahara na marupurupu yake bila kufanya kazi kwa mwaka mmoja
sasa,kwa madai ya Kipande hamtaki.
Ajira za
Upendeleo,
Kama kuna
mgogoro unaofuka Moshi Ndani ya Bandari basi ni huu unaotokana na Ajira za Mhandisi Alois Matei,ambaye ni Naibu
Mkurugenzi mkuu(Maendeleo ya Miundombinu)na mhandisi William Shilla,ambaye ni
mkurugezni wa Uhandisi.Taharifa zilizopo zinasema kuwa Wahandisi hawa wawili
waliajiriwa na Kipande kupitia Mlango wa
Nyuma ,pasipo kufuata taratibu za
sheria.
Huu ni
Mwenderezo wa Unyama unaofanywa na Kipande ndani ya Bandari pasipo kuchukuliwa
Hatua yeyote kutoka kwenye Taasisi za Kupambana na Rushwa TAKUKURU,wala Wizara
husika ya Uchukuzi ambao,mamlaka hiyo iko chini yake.
Huku,Kipande
akinijinadi kwenye mkutano na Uongozi wa mamlaka hiyo,akisema mtu yeyote
atakaye pingana nae anamngoa kwani yeye na mamlaka hiyo ya Bandari hawapati
hasara yeyote bali serikali ndio inapata hasara,na kama yuko mtu yeyeto atakaye
pingana naye(Kipande )basi atamfukuza Kazi.
Duru, hizo
zinasema mzee Kipande amekuwa akifanya Vitendo hivyo vya Kifisadi huku
akijinadi Hakuna mtu wa kumng”oa nafasi hiyo kwa Madai,eti anajuana Kigogo
mmoja aliyoko Ikuru ya Jakaya
Kikwete,ambae amekuwa karibu na Kipande.Ndio maana Amekuwa akifanya Vitendo
hivyo akijua hakuna mtu wakumchukulia Hatua zozote.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni