TAMWA NA MASHIRIKA MENGINE TANZANIA YAAZIMISHA SIKU YA FAMILIA DUNIANI KWA KULAANI VITENDO VYA BOKO HARAMU, CHUKUA MUDA WAKO KUONA JINSI WALIVYOOLAANI VITENDO HIVYO
Mashirika yanayotetea hakiza wanawake na watoto hapa nchini kwa kauli moja wameelaani vikali vitendo vinavyofanywa na kikundi cha Boko haram cha kuwateka watoto wa kike 200 katika maeneo yao ya shule,
Wakitoa tamko lao mapema hii leo jijini Daresalaam kwa Waandishi wa habari, Mashirika hayo yammesema hatua ya kuwateka nyara wasichana si cha kuungwa mkono hata kidogo na kwamba serikali ya Nigeria lazima itafute njia ya kurudisha watoto hao kwa njia yeyeto ile,
"sisi kama mashirika yanayotetea haki za wanawake na watoto nchini Tanzania kwa pamoja na mashirika na wanaharakati barani Afrika tunaungana na nchi nyinginezo Duniani kulaani vitendo vya utekaji nyara kwa wasichana wanafunzi zaidi ya 200 vilivyofanywa na Bokoharam, tunaomba serikali ya Nigeria kufanya kwa kila linalowezekana kuwarudisha watoto hao ambao hawana hatia"Walisema taasisi hizo
Katika hatua nyingine, Mashirika hayo, yametoa wito kwa nchi za kiafrika kuzingatia ulinzi wa rasilimali zilizopo, ambapo amesema rasilimali ndio chanzo chote za migogoro ya namna ya bokoharam ambao mpaka sasa wanateka nyara watu ambao wala hawajui lolote juu ya ugomvi wao na serikali
Wakati huohuo serikali ya nchini Nigeria imewakataria ombi la kiongozi wa boko haram Abubakar Shekau kwa ajili ya kuwaachia huru wanafunzi wa kike zaidi ya 200 waliotekwa na wanamgambo wa kiislam.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa mambo ya ndani alipoulizwa kama serikali itakataa mapendekezo yaliyotolewa na Shekau katika video mpya ambayo wasichana wanaweza kuachiwa huru mara moja endapo Serikali ya Nigeria itawaachia huru wafungwa wote wapiganaji, alijibu kuwa suala katika swali siyo juu ya Boko Haramu kutoa masharti.
Watoto hao wapato 200 walitekwa mwanzo mwa mwezi wa nne na mpaka sasa haijulikani watoto hao walipo, lakini hivi karibuni boko haramu walitoa picha nyingine ikiwaonyesha watoto hao wakiwa tayari wamesilimishwa huku wakiwa wamevalia hijabu.
ABUBAKARI SHEKAU, KIONGOZI WA KUNDI LA BOKO HARAM AKIWA KATIKA MOJA YA POZI LAKE, kKIONGOZI HUYO ALITOA WITO KWA SERIKALI YA NIGERIA KUWATOA WATU WAKE WANAOWASHIKILIA ILI NAYE AWAACHIE WATOTO WA KIKE ZAIDI YA 200. HATA HIVYO OMBI HILO LILIKATALIWA NA SERIKALI YA NIGERIA KUPITIA WAZIRI WAKE WA MAMBO YA NDANI. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni