HAMMADI TAO NANI AMEKUROGA, POSHO ZA LUKUVI ZITAKUUA
Wanaharakati wa kislam hapa nchini wamehoji hatua ya taasisi inayojishugulisha na kujenga undugu kati ya waislam na wakiristo hapa nchini ya kumuomba Mh. Rahis wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuifuta jumuiya ya uamsho na mihadhara wakidai kuwa hatua hiyo inamkono wa mtu na sio bure
Wakizungumza na mwandishi mwandamizi wa mtandao huu hivi
karibuni, Shehe Basareh amesema, kikundi hicho kinatumiwa na wale wote ambao
hawautakii mema uislam.
Amesema kuibuka kwa kikundi hicho na kuanza kumuomba rais
kufuta taasisi ambao ipo kihalali na ambayo haijakutwa na makosa yoyote ya
kuhusika na tuhuma zinazotajwa na wanaotaka kuua uwepo wa taasisi ni wazi kuwa
lengo lao la kutaka kuua viongozi wa kikundi hciho kinazidi kujidhilisha,
Hata huyo anajiita Hammadi Tao, kabla ya kupokea milungura
kutoka kwa huyo mfadhili wake, kwanza angejiuliza kabla ya kuchukua maamuzi
hayo, je kunaushahidiwowote wa kuaminika kuwa JUMUIK imehusika na tuma za
kigaidi huko Zanziabar, Aliosema Basereh
Huko ni kutumika kwa baadhi ya taasisi za kiislamu kuwachafua
waislam wenzao, madhalim wanajua wazi wakiwatumia viongozi wa kidini basi
waislam wataamini hoja zao na kuwafuata, lakini ukweli ni kwamba hao wajenga
udugu wametumika na hakuna wa kubisha katika ukweli huo,
Tunawaomba wale vizuri hizo pesa zao za kuhongwa, waache
kuchafua watu kwani kufanya hivyo ni dhambi kubwa kwa mungu na watachomwa..
Aliongeza.
Hivi karibuni Kikundi cha kujenga udugu kati ya waislam na
wakiristo walimpigia magoti rais na kumuomba kukifuata kikundi cha mihadhara ya kiislam Tanzania
maarufu kama UAMSHO kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kikundi hatari na hakiitakii
mema nchi ya Tanzania
Ombi hilo lilitolewa
na HAMAD TAO ambaye ni mwenyekiti wa
taasisi inayojihusisha na kujenga undugu kati ya dini ya CHRISTIAN AND MUSLIM
BROTHER HOOD SOCIETY ambapo katika mkutano na wanahabari taasisi hiyo imesema kuwa kikundi cha uamsho
hawana lengo nzuri na nchi ya Tanzania kuutokana na matamko yake ambayo imekuwa
ikiyatoa ya vitisho dhidi ya watu mbalimbali pamoja na dini nyingine ambapo amesema
kikundi hicho kinasababisha uhasama baina ya dini na dini.
Katika mkutano huo na wanahabari, HAMAD TAO ambaye ni mwenyekiti wa taasisi hiyo
amesema kuwa kikindi cha uamsho hakina tofauti na vikundi vingine vya kidaidi
duniani huku akienda mbali na na kukifananisha na vikundi kama ALCAIDA,BOCO
HARAM NA ALSHABABU.
“sisi tumekuja hapa kwa upendo na kuipenda nchi yetu
tunaiomba serikali ya Tanzania isiwafungie macho hawa watu wanaounda kikundi
hiki kwani ni hatari kwa amani tuliyonayo”alikaririwa Bw. Tao
Aidha taasisi hiyo imesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kikundi
hicho cha UAMSHO matukio ya kigaidi Zanzibar kama kumwagiana tindikali,makanisa
kuchomwa moto na ugaidi mwingine umekuwa ukiongezeka kwa kasi huku wakikwepa
kuwahusisha uamsho moja kwa moja kuhusika na uhalifu huo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni