UAMSHO HAWATA PONA, MAUAJI YANUKIA
Mjumbe wa uamsho akifafanua jambo, katika moja ya vikao vyake na waandishi wa habari jijini Daresaalam |
Unaweza kusema sasa jumuiya ya uasho na mihadhara ya
Zanziaba r haita pona kufuatia mbegu mbaya inayopandikizwa kwa wananchi na
viongzo wa ngazi za juu hapa nchini kuichukia jumuiya kutokana jumuiya hiyo
kuhusika na matendo ya kigaidi katika shuguli zao za kila leo
Utafiti uliofanywa na mwandishi wa habari hzi umebaini,
utata mkubwa dhidi ya tuhuma zinazoelekezwa kwa jumuiya hiyo, huku wale wote
wanaowanyooshea kidole jumuiya hiyo wakiwa hawana ushahidi wa kusadikika wa
kuwachukulia hatua taasisi hiyo,
Katika kuonyesha kuwa viongzi wa ngazi za juu wamepania
katika mipango ya kuibobomoa tasisi hiyo kwa njia yoyote hata kwa mtutu,
kumeonekana sasa kuna watu wameanza kujitokeza hadharani wakiwahukumu jumuiya
hiyo kuhusika na vitendo vya kigaidi huku wakiwa hawana ushadi wa kutosha dhidi ya watuhumiwa husika
Miongoni mwa viongzoi wakubwa ambao wamejitokeza hadharani
na kuwasema vibaya jumuiya hiyo ya kiislamu hapa nchini ni Mh. William Lukuvi
wakati akimuwakilisha waziri mkuu katika moja ya kanisa huko mjini Dododma,
Katika hotuba ambayo, Waziri huyo wa ofisi ya waziri mkuu
sera na uratibu wa Bunge, amesikika akiwatuhumu jumuiya hiyo, na kuirudia tena
kauli yake katika bunge maalum la katiba pale alipomuunga mkono Mh. Mrema kwa kusema uasho walihusika na vitendo vya
mauaji ya padre, uchomaji wa makanisa pamoja na uharibifu wa miundo mbinu huku
wakijua wazi wanachokisema hawana ushahidi navyo.
Kwa hali ilivyo, na wiwa kusema ili mtu ukitaka umuondoe
katika ramani, ni lazima umfanye asiwe wa thamani katika jamii husika ili hata
kama akiondoka aonekane, na hilo ndilo wanalolifanya viongzoi wakuu wan chi hii
dhidi ya jumuiya ya waislamu ya mjini Zanziabar,
Hivi karibuni, jumuiya hiyo ilikuja juu na kumtaka wziri
huyo kupeleka ushahidi wa tuhuma alizozitoa dhidi yao na kwamba akishindwa
kufanya hivyo basi sheria ichukue mkondo wake, ikiwemo yeye mwenyewe kujiudhuru
ama rais aliyemteua kuichukua dhamana hiyo aliyompa ili kunusuruu vita ya
kidini hapa nchini,
Imeitwa ni vita ya kidini kufuatia ukweli kuwa alihusika
kutoa tuhuma alikuwa kanisani na wanaowatuhumu pia ni wa upande wa pili, sasa
kwa vyovyote vile upande huo wa pili hautakuwa tayari kuona wenzao
wakinyanyasika.
Hebu angalia Mfululi wa tuhuma za uamsho
Mwaka 2004
Jumuiya ya uasho na
mihadhara ya kiislamu JUMUIK ilituhumiwa kuhusika na vulugu zilitokea huko
Zanzibar ikiwemo milipuko ya
mabobu,kuchomwa kwa makanisa,kuchomwa kwa gari ya polisi, na kuharibiwa kwa
miundo, Kufuatia tukio hilo Tume mbili ziliundwa kuchunguza ukweli wa kadhia
hiyo . Tume hizo ni ile ya maziwa makuu na Tume ya kamati maalum ya jeshi la
polisi likiongozwa wakati huo na aliyekuwa mpelezi mkuu wa makosa ya jinai Bw.
Robert Manumba,
Tume hizo mbili mpaka sasa yapata kipindi cha miaka kumi
lakini bado tume hizo zimeshindwa kutoa taalifa yeyote ya utafiti wao kuhusiana
na kadhia ya kipindi kile, japokuwa walitangaza hadharani tume ingeweza
kumaliza majukumu yake na kutoa taarifa
ndani ya kipindi cha mwezi mmoja,
Mwaka 2012
Matukio kama yaleyale ya mwaka 2004 yalijitokeza tena, mnamo
mei 26-29 mwaka 2012 , wimbo ukawa uleule wa kuihusisha jumuiya hiyo ya kiislam
kushiriki katika vitendo vya kiuhalifu huku uthibisho wa ukweli halisi wa
taarifa ukishindwa kuonyeshwa mbele ya jamii, . kufuatia kuandamwaandamwa na kupewa majina mabaya ya
kuhusika na vitendo vya kihalifu mjini Zanzibar, Juiya hiyo ilikaa chini na
kutafakari wanafanya nini ili kutoa ukweli halisi kwa jamii, Ndipo walipoamua
kumuandikia Barua Rais, wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shei mnamo tarehe 03june
2012 ikimuomba rais huyo kuunda tume ili ukweli ujulikane ,
Lakini kwa bahati mbaya mpaka leo hii hakuna tume yeyote
iliyoundwa ili kubaini ukweli wa majina mabaya ambayo Jumuiya hiyo inapewa na
watu wachache ambao hawaitakii mema jumuiya, kutokana na maslahi yao yenyewe
yawe ya kisiasa ama ya kiuchumi,
KAULI YA LUKUVI , MREMA,
Katika hatua ya kushangaza, kiongozi mkuu kabisa wa serikali
ambaye ni waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge, hivi
karibuni ameibuka na hoja zilezile za kuzihusisha jumuiya hiyo ya kiislamu
kuhusika na matendo ya kihalifu akiwa kanisa moja huko Mjini Dodoma,
Lukuvi alikaririwa akimuunga mkono Mh. Mrema kuwatuhumu
Uamsho kuhusika na vitendo vya kiharifu ikiwepo kuuliwa kwa padre, kuchomwamoto
kwa makanisa na uharibifu wa mali za umma na miundo mbinu kitu ambacho waliwahi
kutuhumiwa wakati huo na majibu yake viongozi kuyakaria
Dhana ya uamsho kujihusisha
na chama cha CUF.
Kunatuhuma zingine za jumuiya hiyo kuhusishwa na chama cha
kisiasa wakidai kuwa sera za chama cha CUF zinaendana na sera za Jumuiya hiyo
ya uamsho na mihadhara kauli ambayo katibu mkuu wa jumuiya hiyo Abdalah Said
Ali ameikanusha vikali tena mbele ya hadhala, na sio CUF tu bali jumuiya hiyo
haina uhusiano wowote na chama cha siasa ndani ya Zanziba wala huku bara.
Mjumbe wa jumuiya hiyo ya uamsho ambaye pia ni mkurugenzi wa elimu na habari, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuna mipango inasukwa ya mauaji dhidi ya kikundi hicho, na kwamba siri hiyo imegundulika.
Mjumbe huyo alisema waliogundua uwepo wa mipango ya mauaji ni miongoni mwa polisi ambao wengine tayari wameshacha kazi kutokana na mipango hiyo kuwahudhunishwa
Tumeshaambiwa kuwa kuna mipango ya mauaji, na ndio maana wameanza kwa kutupandikizia uadui kwa raia ili tujulikane sisi ni magaidi, tumejua janja yao tunasema na kuwaomba serikali iachane na mipango ya kuua raia wake
Sina hakika kama Nchi yetu itaingia vitani lakini , kama
hatua za haraka hazitachukuliwa ninaona harufu mbaya dhidi ya uamsho, na hapo
ndipo ninapopaogopa mimi, alisema mmoja wa wadau waliohojia dhidi ya tuhuma
wanazopewa jumuiya ya Uamsho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni