Zinazobamba

BUTIKU AWATAJA MAADUI WA SERIKALI TATU,


Mwenyekiti wa jukwaa la asasi za kiraia na kigoda cha Mwl. Nyerere Foundation Mzee wetu Butiku, akifunguka kwa wajumbe wa jukwaa la asasi zisizo za kiserikali mapema hii leo.Butiku amesema bila kuuma maneno kuwa mchakato wa katiba unachezewa na watu wawili LOWASA na maalim SEIF kwa maslahi yao binafsi
Kwa kile kinachodaiwa ni kuwatolea uvivu  maadui namba moja wa mchakato wa katiba usikamilike kwa amani, mjumbe wa rasimu ya walioba leo hii ameibuka na kufichua mambo mazito huku akiwataja hadhalani wabaya wa mchakato wa katiba ambao wanapinga mchakato wa serikali tatu ulipendekezwa na tume ya rasmu ya katiba

Akitumia, mkutano mkuu wa asasi zisizo za kiraia za ukanda wa maziwa mkuu, mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya licha ya matusi mbalimbali kuelekezwa katika tume hiyo, leo hii ameibuka na kusema ya moyoni huku akionekana wazi kukerwa na vigogo wawili wanaopandikiza chuki kwa wanachama wao ili ibaki serikali tatu waweze kutiomiza matakwa yao ya kisiasa,

Aliyefunguka na kutoa ya moyoni leo hii si mwingine ni bali ni mwenyekiti wa kigoda cha mwalimu Foundation, MZEE WETU Butiku, ambaye amewataja mapapa yanayotaka mchako wa katiba uwanufaishe maslahi yao huku wananchi walio wengi matatizo yao yakiacha solemba,
Amewataja viongozi hao ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika vyama vyao kuwa ni pamoja na Mbunge wa Monduli kupitia chama cha CCM, Mh. edwadi Lowasa, pamoja na katibu mkuu wa chama cha wanachi CUF, na kusema kuwa watu hao wasipobadilika hatima ya serikali tatu hapa nchini ni ndoto.


Butiku ameenda mbali na kusema, inashangaza kuona watu hao ambao wanaushawishi mkubwa sana, wameamua kulivalia njuga suala la serikali mbili huku wao wenyewe wakishindwa kutoa hoja za msingi na badala yake wanatumia watu wanaowaongoza kutumbukiza hoja zao ambazo zinawanufaisha wenyewe,

Butiku amesema tokea mchakato wa kubadili katiba ya wananchi uanze, viongozi hao wameonekana kuupinga, kwa kupandikiza watu wao katika mikutano ya kukusanya maoni, ambapo kumekuwa na mgawanyiko mkubwa wa baadhi ya watu kutoa hoja ambazo zimeonekana wazi kutaka kuwanaufaisha watu fulani,
Walioba alipomaliza kusoma rasimu ya katiba pale bungeni Dododma, Lowasa alinifuata na kuniamkia kisha akasema Kama hoja tu mmejitahidi kujenga, siku ya pili yake katika mazishi pia Lowasa huyohuyo alinifuata tena na kuniambia hata wewe unataka serikali tatu kweli.!!!!!!, nikamwambia hilo ndilo wanaanchi wanataka Asema butiku huku akionyeshwa wazi kukerwa na hali inayoendelea huko bungeni.
wadau wakifuatilia kwa makini sana.

Aidha Butiku ameendelea kubainishwa wazi kuwa rais wa wananhi, JK alishirikishwa kila idara, Jeshi la wananchi nao walishirikishwa kikamilifu na walitoa maoni yao na kwamba uvumi unaovumishwa kuwa jeshi litachukua nchi haina mashiko na badala yake wanataka kuwatsiha wananchi ili wasiweze kupata katiba ya maridhiano ambayo wananchi wanaitaka.
Unakuta mtu anaamka asubuhi anaanza kusema ooh nchi itachukuliwa na wanajeshi, hiyo si hoja , hoja ni kwamba wananchi wanataka nini katika katiba yao, aliongeza Butiku,

Mzee huyo alijipambanua kwa kusema yeye hana mali na amerithi nyendo za Mwl. Kambarage, za kuwatumikia wananchi wa kitanzania, amewaasa watanzania kuhakikishwa kuwa wanajifunga kibwebwe kutetea haki yao la sivyo katiba ambayo itaendaa kuundwa itakidhi matakwa ya watu fulani

Watafiti wa mambo wanasema maarim seif anataka serikali tatu ili aweze kuwa raisi kamili kule zanziba kwani Chama cha CUF ndicho chenye nguvu sana kule Zanziabar, wakati Lowasa anapigania serikali mbili ili awe na nguvu pande zote mbele kama akipishwa kuwa rasi wa jahuri ya muungano.

Hakuna maoni