Zinazobamba

SAKATA LA UKAWA SASA LACHUKUA SURA MPYA, JUKWAA LATIA NENO

MWENYEKITI WA JUKWAA LA KATIBA Bw. Deusi Kibamba akifafa jambo kuhusiana na tathini walioifanya ya mchakato wa katiba kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita,Bw. Kibamba amesema tathimini zinaonyesha mchakato wa katiba uko njia panda na ili kuunusuru maridhiano ya pamoja yanahitajika.Amesema wao wamejitolea kuunusuru mchakato kwa kuomba kupewa fulsa ya kuwa wasuluhishi
 Watanzania wametakiwa kusahau kuhusu suala la kupatikana katiba mpya ndani ya muda ulioahidiwa, hiyo ni kutokana na ukweli kuwa muda huo unaisha kesho na hakuna dalili yoyote ya kupatikana katiba mpya kama ilivyoahidiwa  na Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mh. Mrisho Jakaya Kikwete,

Wakitoa utafiti wao wa kipindi cha miaka mitatu tokea mchakato wa katiba mpya uanze, Jukwaa la katiba limesema mchakato huo wa katiba umekuwa ukigubikwa na changamoto mbalimbali tokea uanzishwaji wake mpaka sasa ambapo kumekuwa na sintofahamu mbalimbali miongoni mwa wabunge,

Akisoma Tamko rasmi la jukwaa la katiba, kutokana na tathimini walioifanywa toka 2010-2014, Mwnyekiti wa Jukwaa hilo Nd. Deusi Kibamba amesema wazi kuwa mchakato huo umeonyesha kubaki njia panda kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya ukawa kutoka nje ya bunge maalum la katiba mapema hivi karibuni
Kibamba amesema, kutokana na mchakato huo kubaki njia panda, wameomba sasa kupewa jukumu la kufanya suluhu kati ya pande zinazolumbana ili watanzania wapate katiba ambayo imelidhiwa pande zote mbili, na kwamba kuonyeshana umwamba miongoni mwa wabunge haitasaidia lolote,
Waandihsi wa habari wakimsikiliza mwenyekiti wa jukwaa la katiba Bw. Deusi Kibamba akifafanua tathimini yao na namna walivyojitoa kuunusuru mchakato wa katiba.
Ameongeza kusema kuwa, kwa tarifa walizo nazo, spika wa bunge maalum la katiba alionyesha nia yake ya kutaka kujenga suluhu kati ya ukawa na Tanzania kwanza, lakini ni wazi kuwa suala la yeye kuwasuluhisha ugomvi huo isingewezekana kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye anayesadikiwa kutokuwa na imani naye,

Amesma Suala la ofisi ya Waziri kuwa wazi muda wote ili kujadili kero za bunge maalum la katiba halina mashiko kutokana na ukweli kuwa, serikali tayari imeshaonyesha upande wake hivyo kuwalazimisha ukawa kwenda katika ofisi hiyo ya waziri ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, mshahara wake kulowa wewe mwenyewe.
Tumeona ili kunusulu tataizo hili ambalo linaweka mchakato wa kupatikana katiba mpya kuwa njia panda, tumeamua kujitolea kuwaleta pamoja pande zinazogombana ili tuweze kukaa nao na kujadili tofauti zao, kisha tujenge suluhu miongoni mwao na mchakato uendelee kama kawaida ,

Anasema, kitendo cha kuupuzia jumla ya wajumbe 200 wasitoe hoja zao katika bunge la katiba ni hatari kwani kunauwezekano yakatokea machafuko kutokana na ukweli kuwa watanzania hawafurahishi hata kidogo na hali inavyoendesha katika bunge maalum la katiba
Katika kuifanya kai hii, tumeamua kuwashirikisha majaji maalufu hapa nchini ambao hawajaonysha kuwa na upande wowote mpaka sasa, kwani tunaamini kuweka watu hao wataweza kujenga suluhu itakayokubaliwa kwa pande zote mbili,
Ikumbukwe kuwa migogoro ya kimaslahi itakuwa mikubwa zaidi ikifika wakati wa kujadili maslahi ya watu, na hivyo lazima kanuni zetu ziweze kuesma kama mtafaruku utatokea nani atakuwa msuluhishi wa pande zinazolumbana, Aliongeza Bw. Kibamba.

Hakuna maoni