maonyesho ya 'kijeshi' taifa yalilenga kuwaziba midomo wadai Tanganyika
Licha ya furaha isiyo kifani waliyopata watanzania siku ya muungano katika uwanja wa taifa, kwa maonyesho mbalimbali ya kijeshi sambamba na maonyesho ya haraiki, wanaharakati wengine waitafsiri sherehe hizo zimelenga kuwaziba midomo wanaharakati wanaodai serikali tatu hapa nchini,
Wakizungumza na waandihsi wetu mapema hii leo katika mahojiano maalum na mtandao huu, wananchi katika jiji la Daresalaam, wametaja hatua ya jeshi la tanzania kupeleka vifaa vya kijeshi sambamba na maonyesho yaliojaaa ubabe na kujihami kwa hali ya juu kuwa yalilenga kuziba midomo ya watu fulani wanaodai Tanganyika yao,
Wamesema kwa hali yakawaida madege ya kivita, maonyesho ya kivita, sambamba na vifaa vya kivita kama vile visingeweza kuonyeshwa katika mazingira yale ikizingatiwa kuwa siku ile ilikuwa ni siku ya furaha kwa watanzania kufikisha miaka hamsini ya muungano wetu kwa amani
Wameongeza kusema kuwa, kauli za viongzoi wa juu ambao wamekuwa wakiimba kila leo kuwa Jeshi litakuwa nchi kama hawakuwa makini ndiyo iliyojidhilisha siku ya muungano ambapo, jeshi la wananchi lilikuwa likionyesha ukakamavu wake kwa wananchi katika siku hiyo ya sherehe,
Tunadhani kama kulikuwa hakuna haja ya kupeleka vifaulu katika uwanja wa taifa, kwani pale hakukuwa na vita na badala yake tulikuwa tunasherehekea muungano wetu ambao ndio kimsingi unajenga utanznaia wetu' iweje sasa tuwekewe vifaa vya kivita na kututisha kama vile, Aliongeza mmoja wa waliohojiwa katika mahojiano maalum na Mtandao huu
Aidha wadau hao walipendekeza kwa silikali kutenga siku maalu ya maonyesho ya kijeshi ili watanzania wanaotaka waende kuangalia maonyesho hayo kwani kimsingi yanaonyesha uwezo wa jeshi letu kutulinda na maadui wawe wa ndani ama wa nje.
Kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na viongzo kuwa jeshi linaweza kuchukua nchi zimekuwa za kawaida katika siku za hivi karibuni ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa wamekuwa wakikaririwa kusema maneno hayo mbele za hadhara.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni