RUBADA WAPATA BODI MPYA,CHIZA AWATAKA WAINASUE MAMLAKA HIYO
Na mwandishi wetu,
Waziri wa Chakula na Kilimo, Mh. Cristopha Chiza ameitaka
bodi mpya iliyoingia madarakani katika
mamlaka ya maendeleo yam to rufiji (RUBADA)kuhakikisha wanafanya jihida za
kuikwamua mamlaka hiyo ambayo kwa sasa imeonekana kama haina faida miongoni mwa
macho ya watanzania ambao wanaona majuku mengi ambayo yanayofanywa na mamlaka
hiyo tayari tayari zinafanyawa na taasisi zingine,
Akizungumza na bodi hiyo mpya alioizindua mapema hii leo, Dk
Chiza amesema kazi kubwa ambayo bodi hiyo inayo kwa sasa ni kubadilisha taswira
ya mamlaka hiyo ambayo kwa sasa siyo
nzuri kutokana kuonekana kama haina umuhimu kufuatia kazi zake kutojulika na
hata mipaka yake ya uwajibikaji kutokuwa wazi,
Chiza amesema, lazima wahakikishe kuwa taswira hiyo ya
kudhaulika hadi kufikia hatua ya baadhi ya watu kupendekeza kufutwa kwa mamlaka
hiyo inabadilika na kuwa mamlaka yenye meno na kusimamia vizuri majuku yake
katika maeneo ambayo yataainishawa ,
Najua mnaingia katika mamlaka hii mkiwa na kazi nzito ya kubadilisha taswira ya
mamlaka na kuifanya mamlaka itakayosaidia serikali kwa kuhakikisha mnatunga
muswada wa sheria utakaohakikisha mnapewa majukum yenu ya kuyasimamia ipasavyo,
ili muweze kuonyesha kazi mnayofanya kwangu na kwa rais kwa ujumla. Aliongeza
Dk Chiza.
Aidha Chiza ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa karibu na
utawala uliopo ili kufikia malengo ya kuiboresha taasisi hiyo kwani kwa kufanya
kazi pamoja kutaleta tija katika utekelezaji wa majukum ya kila leo ya Mamlaka,
Naye Mwenyekiti wa bodi hiyo ya Rubada Prof. Msambichaka Lucian, amesema kuwa
wamechukua changamoto ambayo imetolewa na Mh. Cheza na kwamba kwa kuanzaia
wameamua kuanza kujipa malengo ya kupeleka taarifa ya utekelezaji wa majukum
yao ya kila kwa waziri kila baada ya
miezi mitatu ili kumuonyesha waziri ni namna gani wamejipanga kuifufua taasisi
hiyo ambayo ilikuwa inaelekea kufa,
Kwanza tunashukuru kwa muheshimiwa waziri kutambua
changamoto iliyo mbele yetu, lakini tunamuhakikishia muheshimiwa huyo
uwajibikaji wa kiwango cha juu, ili asione kama kuteua bodi hii amefanya makosa
ya hali ya juu,
Tunafahamu kuwa changamoto ni kubwa ya kuondoa matatizo
katika sekta hii ya kilimo lakini tumejipanga kuondoa vikwazo vyote, kwa
kuanzia tutaandaa muswada ambao kama waheshimiwa wabunge wataupitisha basi
tunadhani hii tabia ya muingiliano wa majukum kati ya wizara moja na nyingine
itaisha,
Utaona hapa Lubada, tumefanya tafiti nyingi nzuri lakini
hakuna anayetumia tafiti hizi na watu wanaamua kuanza kuandaa tafiti zingine
wakati hapa tafiti zipo tena za kitu hichohicho wanachofanyia tafiti, tunadhani
kutokuwa na muundo mzuri wa uwajibikaji ni tatizo na ndio maana sisi tumeletwa
kuondoa sintofahamu hiyo katika mamlaka hii, Aliongeza Prof. Lucian
Naye mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya RUBADA Bw. Aloyce L.
Masanja, ametaja changamoto nyingi zinazoikabili taasisi hiyo kwa sasa, moja
wapo ikiwa ni muingiliano wa majukumu kati ya kituo cha uwekezji na mamlaka
yake hatua ambayo inaonyesha wazi kuwa kuna haja ya kufanya marekebisho makubwa
ya sheria iliyoipa mamlaka taasisi hiyyo
kuanzishwa kwake,
Amesema muarobani wa kuinasua RUBADA kwa sasa ni kuundwa kwa
sheria mpya ya mamlaka itakayoweza kuainisha kazi zao ili kazi zao zisiweze
kuingiliana na mamlaka zingine
mwishoooo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni