WADAU WASEMA JUKWAA LA KATIBA HALINA SIFA YA KUSULUHISHA MGOGORO BUNGE LA KATIBA, MGEJA NAYE ATIA NENO
Sifa pekee ya refarii, ni kuwa mtu ambaye
hana mapenzi na moja ya pande ambazo wanapambana katika soka, Kama ikitokea refarii
huyo anakuwa na upande ambao anaushabikia basi refaa huyo huambiwa amepoteza
sifa ya kuwa refa na hivyo jitihada za kutafuta refa mwingine kuchezesha
mpambano huo itachukuliwa,
Katika masuala ya soka hali hiyo ni ya kawaida
sana, Tumeshuhudia baadhi ya klabu maarufu sana hapa nchini zikiingia katika
mgogoro wa refarii, wengine wanasema huyo ni refa wa Yanga, Huku nao simba
wakisema huyo ni refa wa simba, timu singine utasikia huyo refa kapewa mlungura
basi imekuwa ni hivyo kila mmoja hana imani na refa ambaye amejimbambanua kuwa
na upande ambao anaushabikia,
Hivi karibuni Jukwaa la katiba hapa nchini,
lilijitokeza hadharani na kutangaza kuomba fulsa ya kuwa wasuluhishi wa
migogoro itakayokuwa ikiibuka pale mjengoni, mjini Dododma,
Jukwaa walifikia hatua hiyo baada ya kuona
kutokuelewana kati ya ukawa na wajumbe wengine katika bunge maalum la katiba,
huku wakisema wazi kuwa kutokuelewana huko hakutoishia tu kwa ngazi ya ukawa na
Tanzania kwanza, kwani huko mbele tunakoenda inaonekana wazi kuwa migogoro
itakuwa mikubwa isivyo kawaida kutokana na ukweli kuwa maslahi ya watu yataanza
kujadiliwa ,
Wakulima watatetea maslahi ya kundi lao,
wafugaji watatetea maslahi ya kundi lao, huku wabunge wa kisiasa nao watatetea
maslahi ya ukomo wao wa kuwa wabunge hapo ndipo mgogoro wenyewe utakapoanza na
huku nje kanuni na sheria zote zikiwa kimya juu ya migogoro hiyo itakapotokea
itapelekwa kwa nani,
Kufuatia hali hiyo jukwaa wameliona hilo na
wamekuja na muarobaini wa kuomba tenda ya kuwa wasuluhishi wa migogoro yahapo
mjengoni, wameanza kuwaleta kundini majaji maarufu ukanda wa Afriaka mashariki
na kati na Dunia kwa ujumla, ambao kwa muda mrefu hawajaonyesha kuwa upande
fulani ili kufanya kazi nao ya kutatua migogoro ya Mjengoni
Miongoni mwa majani ambao wamewaleta kundini
ni pamoja na Jaji Banabasi Samata, ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya katika
mchakato huu wa katiba na hajaonyesha wazi kwa jamii kuwa yeye yuko upande
gani, hatua ambayo imeonyesha wazi kuwa yeye ni refarii mzuri katika suala
migogoro,
WANANCHI WAHOJI UHALALI WA JUKWAA KUWA
REFARII
Licha ya nia yao njema ya kuhakikisha
migogoro katika bunge maalum la katiba yanapatiwa ufumbuzi, bado wananchi
wamejitokez ana kusema waziwazi na mtandao huu kuwa jukwaa la katika halina
sifa ya kuwa refarii wa mchakato kutokana na ukweli kuwa tayari wameonyesha
upande ambao wanaushabikia
Wakizungumza na mwandishi maalum wa Mtandao
huu hivyi karibuni, mmoja wa wanaharakati makini sana, ambaye hakutaka majina
yake kutajwa katika mtandao huu amesema, tokea azaliwe na kuanza kuisikia
itikadi ya jukwaa la katiba haijawi hata siku moja kuonyesha wazi kutaja hata
mazuri yanayofanywa na serikali ya chama cha
CCM, hatua anayoitafsiri kuwa Jukata tayari wana mlengo katika kufanya
kazi zao,
Amesema Chama cha mapinduzi hakiamini kama
JUKATA wanaweza kuwa wasuluhishi wazuri wa migogoro itakayotokea kule bungeni,
na badala yake watakuwa wanapendelea kina ukawa, na kukandamiza hojaza CCM
hatakama zinamashiko kiasi gani,
Kufuatia ukweli huo ni wazi kuwa tayari haki
ya wao kuwa marefa imepotea kama wao JUKATA walivyotangaza kuipoteza haki ya
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa mmoja wa wasuluhishi wa migogoro
,wakidai kuwa rais amepoteza sifa hiyo kwa kuingilia mchakato na kutangaza nia
yake hadharani ya kutetea serikali mbili ya chama chake
Amesema hata kama kuna vitisho kiasi gani
kuhusiana na kupotea kwa amani na kufanyika kwa machafuko hapa nchini kutokana
na kutokuwepo kwa msuluhishi ni bora kuliko kuwa na msuluhishi ambaye tayari
ameonyesha ushabiki wa wazi wa upande fulani,
Tunadhani kuna haja ya kuwepo wasuluhishi
hata kama wanatoka nje, lakini hawa JUKATA wamepoteza sifa nahivyo hawastahili
kubeba jukumu hilo zito ambalo kama watapewa watu kwa kutoangalia vigezo maalum
tunaweza kuongeza tatizo kuliko kutatua tatizo kama JUKATA wanavyosema.
Aliongeza
MGEJA AFUNGUKA,
Kwa upande wake mwasiasa nguli wa CCM , Toaka mkoa wa Shinyanga, Bw. Khamis Mgeja amebuka na kusema kuwa hatua iliyotangazwa na Jukwaa la katiba ni ya kupongezwa na kwamba wanastahili kupewa jukumu hilo kama kweli wamedhamilia kuondoa migogoro katika mchakato wa uundaji wa Katiba mpya,
Amesema mchakato wa katiba mpya si wa mtu ama chama fulani bali ni mchakato wa wote na kwamba mchakato ukiharibika asijekuonyeshewa kidole mtu yeyeto kwani saa ya kufanya marekebisho ni sasa, kusbuli hali iwe tete hakutaleta tija hata kidogo .
Katika hatua nyingine Mgeja ametoa wito kwa wafuasi wa ukawa na wale wajumbe wa ukwa kuachana na tabia ya kususa, kwani tabia hiyo haitajenga katiba na badala yake basi wajipime ni namna gani wanaweza kujenga hoja na kuwashawishi wenzao ili waweze kukubaliana kwa hoja na sio kuwa na msimamo ambayo haitakuwa na tija kwa mustakabali wa katiba mpya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni