Zinazobamba

ATHARI YA KAULI YA PINDA BUNGENI HII HAPA, DCI MNGULU ABANWA MBAVU


Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Isaya Mngulu ambaye pia ni mkurugenzi wa makosa ya jinai hapa nchini, akitoa neno kwa niaba ya IGP Ernest Magu mapema hii leo, Mngulu amesema, watanzania wanapaswa kufuata utii wa sheria, kwani kujichukulia sheria mkononi haivumiliki.
Utafiti uliofanywa na kituo cha binadamu kuhusu  haki za binadamu kwa raia wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka huu,ubebaini ya kuwa haki za binadamu kwa tanzania zimekuwa haziheshimiwi kwa kiasi kikubwa huku ikitajwa moja ya sababu ya kutoheshimu haki za binadamu ni kuwa kauli ya waziri mkuu wa Tanzania, Bw. Mizengo Pinda aliyoitoa bungeni dodoma hivikaribuni,

Akisoma taarifa hiyo ya haki za binadamu, mtafiti mkuu wa taarifa hiyo, Bw. Pasience Mlowe, aliyesaidiana kwa karibu na Mr. Paul Mikongoti alisema taarifa hiyo imeonyeshwa kwa kiasi kikubwa kukiukwa kwa haki za binadamu unaoofanywa na jeshi la polisi hapa nchini hususani katika zoezi zima la tokomeza ujangili namba moja na namba mbili liliofanywa hivi karibuni

Mlowe amesema, katika taarifa hiyo, imegundua uvunjwani wa hali ya juu ya haki za binadamu katika mazoezi yote ya kutokomeza ujangili na kwamba sababu inajwa kuwa ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na kauli ya waziri mkuu aliyotoa bungeni,

Ikumbukwe kuwa waziri mkuu aliwahi kusema kuwa, wapigwe tu wanaokaidi sheria hali iliyowapa fulsa watekelezaji wa zoezi la tokomeza ujangili kuingia katika zoezi hilo wakiwa na hamu ya kupiga, kunyanyasa, na kuwatenda vitendo ambavyo si vya kiungwana raia katika maeneo yao ya kazi
Mtafiti mkuu wa ripoti ya mwaka juu ya haki za binadamu iliyofanywa na kituo cha haki za binadamu akifafanua jambo mbele ya wadau waliohudhulia katika sherehe ya kuzindua taarifa hiyo katika viwanjwa vya kituo cha haki za binadamu
Baadhi ya wadau wa haki za binadamu wakifuatia kwa makini katika uzinduzi huo wa taarifa ya haki za binadamu, taarifa hilyo imebaini kwa kiasi kikubwa haki za raia kuchezwa na hakuna anayejali mwaka hadi mwakia,

Mkurugenzi wa kituo cha hakiz za Binadamu, Bi. Kijo Bisimba akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, mapema hii leo katika viwanjwa vya kituo cha haki za binadamu, katika uzinduzi huo, reporti iligawia kwa watanzania wote waliohudhulia katika uzinduyzi huo. 
Isaya Mngulu akizindua taarifa hiyo ya haki za binadamu mapema hii leo.

Hakuna maoni