wadau wailalamikia ikulu, soma ujue ni kitu gani hicho...
Na Edson Kamukala
ARGUE, don’t shout (Jenga hoja, usipige kelele). Hivi ndivyo
wasomi wabobezi wanatutaka tufanye katika kujadili masuala. Hatupaswi kutunisha misuri, kupayuka, kutweta na kutukana ama kubishana pasipo kuonesha ushahidi wa vielelezo.
Wahenga wanasema kwamba; lisemwalo lipo na kama halipo basi laja. Kwa bahati mbaya sana tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, viongozi wake wengi wamekuwa wakikurupuka kujibu na kukanusha hoja nzito zinazoelekezwa kwa serikali wakidhani wamezima mjadala.
Kila serikali inapotuhumiwa ama Rais Kikwete mwenyewe, mara moja utawasikia viongozi mbalimbali au Idara ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, wakitoa matamko makali ya kukanusha tuhuma husika wakisema ni ujinga, upuuzi na upotoshaji wa makusudi.
Hata pale ambapo tuhuma zenyewe zinakuwa na ukweli kwa
asilimia fulani, wasaidizi hao hawajipi muda wa kutafakari na
kujiziuliza ni kwanini awe yeye au serikali yake ndipo wakanushe na hatimaye kuchukua hatua badala ya kuishia kusema ni upuuzi, uzandiki na uongo mtupu. Je, inatosha kuendelea kutoa matamko ya hasira ya kukanusha ama tujifunze kujenga hoja kwa vielelezo kisha tuchukue hatua badala ya kupiga kelele za kujifedhehesha wenyewe?
Mwaka 2006, mwandishi wa kimataifa, Hubert Sauper, alitengeneza
filamu nchini Tanzania eneo la Ziwa Victoria, mkoani Mwanza na kuipa jina la The Darwin’s Nightmare. Filamu hiyo ilipata baraka za vibali kutoka kwa taasisi husika za serikali hapa nchini ambapo mtunzi wake alilenga kuonesha jinsi samaki wanavyokwisha Ziwa Victoria baada ya kuwepo mfumko mkubwa wa viwanda vya
minofu ya samaki jijini Mwanza na hivyo kuwafanya wakazi wake kushindwa kula tena kitoweo hicho.
Sauper alionesha jinsi wakazi hao wanaovyoishi kwa kutegemea
kula masalia ya vichwa vya samaki maarufu kama ‘mapanki’ vinavyotupwa kutoka viwandani vikiwa na wadudu, hivyo kuwepo uwezekano wa kuhatarisha afya zao.
Waliobahatika kuitazama filamu hiyo, wakiwemo viongozi wetu
walimwona mwandishi mwandamizi nchini, Richard Mgamba, aliyekuwa akimsaidia Sauper kutafsiri kwa Kiingereza ushahidi uliotolewa na wakazi waliohojiwa.
Hakuna aliyekuwa ameona kasoro katika filamu hiyo, ambayo
baada ya kushinda tuzo kadhaa nje ya nchi ndipo serikali ilizinduka
usingizini ikitoa matamko ya kukanusha ikidai hakuna jambo kama hilo, bali Sauper ni mzandiki, mpuuzi na mzushi.
Mara tu baada ya Rais Kikwete kutoa utetezi huo, Chama Cha
Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza kikaandaa maandamano yaliyoitwa ya kuunga mkono kauli ya rais kuhusu filamu hiyo, huku wakimsonga na Mgamba kuwa si raia wa Tanzania ndio maana alitumika kutafsiri katika kuichafua
serikali.
Nakumbuka wakati huo nilikuwa mkoani Mwanza nikiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), ambapo siku hiyo nilipata taabu kuwaelewa viongozi wa CCM na wafuasi wao. Zaidi nilikuwa nikijuliza waliandamana kupinga nini?
Kwamba si kweli hawali mapanki au walikurupuka tu kwa sababu Rais Kikwete ambaye anatokana na chama chao kasema? Kesho yake nililazimika kwenda katika baadhi ya maeneo yanayotajwa kwenye filamu hiyo na kuzungumza na wakazi kadhaa wakakiri kuwa wanakula mapanki.
Septemba 2011, mtandao maarufu wa Wikileaks ulichapisha habari zikimnukuu aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer, akidai Rais Jakaya Kikwete alipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa tajiri wa Falme za Kiarabu anayemiliki Hoteli ya Kempinski ya jijini Dar es
Salaam, Ali Albwardy.
Wikileaks ilidai kuwa Rais Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na baadaye rais aliwahi kufadhiliwa na tajiri huyo kwenda London kwa ajili ya kufanya manunuzi ya suti tano.Kwamba alichangisha na kupokea fedha za kampeni za CCM kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2005 uliomweka madarakani.
Kutokana na tuhuma hizo ambazo hata hivyo siwezi kuthibitisha kama zilikuwa za kweli au hapana, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilijitokeza kukanusha ikisema: “Ni uongo na upuuzi. Ni uongo mtupu ambao una lengo la kuchafua jina la rais. Tunasikitika kwa kuona jina la thamani la balozi linahusishwa na umbeya wa kijinga kiasi hiki.”*
Kama ilivyofanyika kwa mtayarishaji wa filamu ya ‘mapanki’
ndivyo ilitokea pia kwa Wikileaks kwani tulikanusha tu kwa maneno makali, hatukuonesha upande wa pili wa ukweli wa tuhuma wala kuwachukulia hatua za kidiplomasia waliohusika kuichafua Tanzania na rais wetu kama ulikuwa uongo.
Baadaye ndipo tukashuhudia wanyamapori wetu akiwemo twiga
wakitoroshwa kwa kupandishwa kwenye ndege ya kijeshi ya Shirika la Ndege la Falme za Kiarabu bila wacheza ‘mchezo’ husika kuonwa na vyombo vyote vya dola vilivyokuwa uwanjani hapo siku ile.
Kwa waliosikia tamko la Ikulu la kukanusha tuhuma za Wikileaks
bila kuchukua hatua, kisha muda mfupi baada ya hapo wakasikia kuwa wanyamapori wetu waliibwa mbugani na kuswaga hadi Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) halafu wakatoroshwa kwa ndege ya kijeshi kwenda Uarabuni, wanabaki na picha gani?
Lisemwalo lipo, kama halipo basi laja. Februari 9, 2014, gazeti
la Uingereza la Daily Mail (toleo la Jumapili) la Mail on Sanday,
kupitia kwa mwandishi wake, Martin Fletcher, lilichapisha makala iliyoituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa inawalinda watu
wanaojihusisha na biashara ya ujangili.
Mwandishi wa makala hiyo akaenda mbali zaidi na kuihusishs Idara ya Usalama wa Taifa, baadhi ya wanafamilia wa karibu na Rais Kikwete, wanasiasa wa ngazi za juu serikalini na vigogo wa CCM.
Kama hiyo haitoshi akadai kuwa ndege iliyomleta Rais wa China
alipotembelea Tanzania mwaka jana, iliondoka na shehena ya pembe za ndovu.
CCM inatajwa kwamba serikali yake inaachia biashara hiyo kwa sababu inatafuta fedha za kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, lakini aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, anadaiwa kuwa alikuwa mwadilifu na kwamba aliwahi kuwasilisha majina ya majangili kwa rais ila hadi anag’olewa hayakuwa yamefanyiwa kazi.
Hizi ni tuhuma nzito na zinazoweza kuifedhehesha nchi na rais
wetu kama itathibitika ni za kweli. Kwa bahati mbaya badala ya serikali kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua, Ikulu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, walikanusha tu wakidai ni upuuzi,uzandiki na uongo mtupu.
Siku chache baada ya kuambiwa ni uongo mtupu, Rais Kikwete
akakaririwa akiwa mjini London akisema kuwa wanayo orodha ya majina 40 ya mtandao wa ujangili nchini pamoja na kinara wao aishie jijini Arusha. Je, inatosha kuendelea kukanusha tu ama tuchukue hatua? Tafakari

Hakuna maoni
Chapisha Maoni