JUKWAA LA KATIBA KUONGOZA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI KATIKA KUPATA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA, WENYEWE WASEMA WATAPELEKA WAJUMBE 20 KWA MH. RAIS KIKWETE
Na mwandi wetu,,
Daresalaam
Daresalaam
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makinitaarifa ya kaimu mwenyekiti juu ya kuwaongoza taaasisi zisizo za kiserikari NGOS, kuteua wajumbe 20 katika bunge la katiba. |
SIKU chache
baada ya Rais Jakaya Kikwete kuitisha
makundi kupeleka mapendekezo ya majina ili aweze kuteua wajumbe wa Bunge la
Katiba.Nalo Jukwaa la Katiba nchini limechukua hatua ya kuongoza Taasisi zisizo
za kiserikali katika kuteua wajumbe hao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo kwenye ofisi za Makao makuu ya Jukwaa la Katiba
nchini jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa jukwaa hilo Hebron Mwakagenda
amesema Jukwaa hilo la katiba limeamua kuchukua jukumu la kuongoza taasisi
zisizo za kiserikali katika hatua hii.
“Jukwaa
la
katiba limechukua hatua ya kuongoza Taasisi zisizo za za kiserikali na
pia
tumeandaa mkutano mkubwa utakaofanyika New Dodoma Hoter tarehe 30 mwezi
huu, tunataradadi mkutano huu utakaoudhuriwa na wajumbe wapatao
200 toka kila mkoa na wilaya za Tanzania Bara na Zanzibar”alisema
Mwakagenda.
Vilevile
Mwakagenda aliongeza na kusema dhumuni la mkutano huu ni kuchagua wajumbe wanaopenda kuingia kwenye Bunge la katiba.
“Mkutano huu
tutakua na kazi ya kuchagua wajumbe wanaopendekezawa kuingia kwenye Bunge la katiba ili kumwezesha Rais kuteua
wajumbe 20 miongoni mwao kwa mujibu wa sheria ya Mabadiriko ya katiba sura ya 83
ya mwaka 2013”
“Mara baada
ya zoezi la uchaguzi wa wajumbe tutamwandikia barua Rais kumsihi aweze kuteua
wajumbe 9 kutoka kwenye uwakilishi wa kijiografia na wajumbe na wajumbe 11 kutoka kwenye uwakilishi wa
kisekta ili kuwa na uwakilishi mpana”alifafanua Mwakagenda.
Katika hatua
nyingine Jukwaa hilo la Katiba hapa
nchini limewataka makundi mengine yaliyotajwa kwenye sheria,kuitisha mikutano
ya kidemokrasia kuchagua wajumbe wao na kuyapeleka kwa Rais kikwete ili aweze kufanya uteuzi wa mwisho.
Tamko hili
la Jukwaa la katiba limekuja baada taarifa iliyotolewa na Ikuru ikonyesha
mwisho wa kupeleka majina ni tarehe 2 mwezi ujao.Na makundi hayo
yaliyobainishwa kwenye sheria ni,Taasisi zisizokuwa za Kiserikali,Taasisi za
kidini,vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu,Taasisi za Elimu ya Juu,
Makundi yenye ulemavu,Vyama vya wafanyakazi,Vyama vya wafugaji,Vyama vya
wakulima na vyama vinavyowashirikisha wavuvi.
VIGEZO VYA KUWAPATA WAJUMBE 20 TOKA TAASISI MBALIMBALI ZISIZO ZA KISERIKALI
Akizungumzia namna ya kuwapata wajumbe wajumbe 20 toka taasisi mbalimbali, Mwakagenda amesema tayari wameamua kuitisha mkutano mkubwa wa taasisi zisizo za kiserikali mjini dodoma kujadili suala hilo,
Wajumbe watapatikana kwa vigezo vya uwakilishi wa kiigeografia, katika kipengele hiki kutakuwa na uwakilishi wa kanda ya ziwa, ambako kuna mikoa ya Kagera Mwanza, Geita,Simiyu na Mara,
Kanda ya kati kutakuwa na mikoa ya Singida,Dodoma,na Morogoro, wakati kanda ya Magaharibi kutakuwa na mikoa ya Shinyanga Tabora,Katavi, na Kigoma
Kanda nyingine ni kanda ya Pwani itakayokuwa na mikoa ya Daresalaam na Pwani yenyewe,
Kanda ya kaskazini kutakuwa na mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Manyara,na Tanga, Kanda ya nyanda za juu kusini Kutakuwa na mikoa ya Iringa Njombe, Mbeya na Rukwa, kanda ya kusini kutakuwa na mikoa ya Ruvuma,Mtwara, na Lindi
Kanda zingine ni Kanda ya Unguja amboyo ina mikoa yote ya unguja na kanda ya mwisho ni kanda ya pemba yenye mikoa yote ya Pemba.
No comments
Post a Comment