KINANA ANAPOLIA NA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA SERIKALINI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Masoko ,kijiji cha
Lupando wilaya ya Rungwe ,Katibu Mkuu waliwaambia wananchi hao kuwa
urasimu na umangi meza wa watendaji wa serikali ndio unachangia kwa
kiasi kikubwa kurudisha maendeleo yao nyuma na kusema kamwe CCM
haitokubali hali hiyo iendelee na kusisitiza CCM itahakikisha wananchi
wanapata haki zao za msingi kwanza.

Mwakilishi wa Wananchi wa
Kijiji cha Lupando Ndugu Wema Mwaipopo akiomba sana kwa niaba ya
wananchi wake watatuliwe suala la maji,umeme na barabara kwani hizo ndio
zilikuwa ahadi kubwa za Mbunge na Rais.

Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Masoko kijiji cha
Lupando na kuwaambia wananchi kuwa wapinzani ni sawa na Jogoo hata aamke
saa ngapi hawezi fungua mlango,na kuwasisitiza wananchi wa kijiji hicho
ni CCM pekee inayoweza kuwazungumzia na kero zao zikatatuliwa.

Asumwisi Asagwile Mwatebela
,Mlezi wa Vijana wa Chadema wilaya ya Rungwe akirudisha kadi yake kwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga rasmi na CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiwira Rungwe na wakati wa
ufunguzi wa vikundi viwili vya wajasiriamali ambapo aliwaambia vijana
maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na waondoe mawazo kuwa
Katiba mpya ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yao.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya shule ya Sekondari ya Ikuti
ikiwa moja ya sehemu ya ahadi ya serikali ya kujenga maabara katika kila
shule ya Sekondari ya Kata.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Ikuti wilayani Rungwe.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahmani Kinana akiongozana na Mkuu wa Shule ya Ikuti Ndugu Emmanuel
Ngasa pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali baada ya kukagua
jengo la hosteli la shule ya sekondari ya Ikuti.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina namba 2,Butonga Tawi
la Ikuti kwa Balozi James Mbasi, na kusisitiza viongozi wote wa CCM
waige mfano wa Mabalozi kwani wanafanya kazi kwa kujitolea katika
kukiimarisha na kukijenga chama.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahama Kinana akikata utepe kama ishara ya kuwasha umeme katika
kituo cha Afya cha Ikuti wilayani Rungwe.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa wilaya ya Rungwe pamoja na
wananchi kuelekea kwenye uwanja wa mkutano Ikuti.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya Wilaya Ndugu Richard Kasesela akipiga ngoma ya Kitongo kabla ya
kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ikuti ambapo mgeni rasmi
alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Mbunge wa Viti Maalum
Wananwake mkoa wa Mbeya Dk.maru Mwanjelwa akicheza ngoma kabala ya
kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ikuti ambapo Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa kitaifa
aliofutana nao Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose
Migiro na Katiibu wa NEC Itikadi na Uenezi walihutubia.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa
wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akihutubia wakazi wa kata ya Ikuti na
kuwaambia wanawake waandae vikundi vyao kwani Benki ya wanawake karibia
itafunguliwa hivyo fursa za kupata mikopo zitaongezeka na kusaidia
kufanya biashara kwa ufanisi na kuleta maendeleo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ikuti wilayani Rungwe mkoa wa
Mbeya na kusema serikali ipunguze matumizi yasiyo na lazima na badala
yake nguvu nyingi iletwe kwa wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Wakazi wa Ikuti wakiwa juu
ya mti wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao ambazo nyingi
zilijibiwa vizuri hasa suala la umeme ambalo wananchi wanaweza kulipa
kidogo kidogo.

Dk.Mary mwanjelwa
akizungumza na akina Mama wauza ndizi wa kijiji cha Iponjola kata ya
Rufingo wilaya ya Rungwe na kuwataka waanzishe vikundi kwani benki ya
wanawake ipo karibuni kufunguliwa katika mkoa wa Mbeya hivyo itawasaidia
kupata mikopo kwa riba nafuu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alisimama kuwasalimu wakina mama hao kisha kuutambulisha uongozi wote aliokuwa nao kwenye msafara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alisimama kuwasalimu wakina mama hao kisha kuutambulisha uongozi wote aliokuwa nao kwenye msafara.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni