CHADEMA WAMJIBU ZITTO NA WENZAKE, WASEMA
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CHADEMA, AKIFAFANUA JAMBO |
SIKU chache baada ya
aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kikushutumu chadema kwa
uamuzi wa kumvua uongozi aliokuwa nao ndani ya chama hicho.
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo “chadema” kimeibuka na kumpa ukweli wake,Ukweli wa chama hicho
ulitorewa na Mwanasheria wa Chama hicho,ambaye ni
Mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Lissu pamoja Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la ubungu John
mnyika,leo makao makuu ya chama hicho jijini dar es salaam wakati wakizungumza na wahariri pamoja na
wandishi wa habari
Kuhusu sababu ya kumvua
uongozi ndani ya chadema
Kuhusu hoja ya kumfukuza chadema
mwanasheria wa chama hicho Tundu lissu alisema uamuzi waliofanya ulikuwa sahihi
na wamefuata kanuni zote za chama kwa mwanachama au kiongozi yeyote anayeenda
kinyume na taratibu za chama
“Sheria zipo wazi na sheria
hizi sijatunga mimi wala zitto,sheria hizi ni Chama,kwa kiongozi yeyote au
mwanachama akifanya mambo kinyume, kamati kuu ya chadema inanguvu ya kumvua
uongozi na ikwezekana hata kumfuta uanachama na kamati kuu ya chadema
haijavunja katiba”alisema Lissu
Vilevile mwanasheria huyo
akafafanua kuhusu hatua ambazo chama kinachofanya kwa mda huu baada ya kumati
kuu ya chadema kuvua uongozi wa chadema zitto kabwe pamoja na mjumbe wa kamati
kuu wa chama hicho Dk kitilo Mkumbo
“Kwa sasa chama teyali kimekamilisha utaribu
wa kuwapa barua kwa maandishi kama katiba ya
chama inavyosema na vilevile chama kimewapa fursa ya siku kumi ili waje
kujitetea kwenye tena kwa maandishi juu ya tuhuma zinazowakabili kwenye kamati
kuu ya chama na chama kitasikiliza na kutoa maamuzi”alizidi kufafanua Lissu
Aidha Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la ubungu John
mnyika alisema kama wathumiwa hawo watadharau
maamuzi ya chama kuhusu kuja kujitetea baada ya siku kumi na nne basi chama
hicho kitafanya maamuzi magumu
“kama siku kumi na nne zikipita watuhumiwa
hao hawatafanya busara kuja kujitetea kwenye kamati kuu ya chadema kwa maandishi
kama katiba ya chama inavyosema, basi chadema
itafanya maamuzi magumu kwa sasa sitaweza
kuzungumzia hatua tutakazochukua”alisema John Mnyika
Suala la waraka wa siri
Kuhusu
walaka wa siri ambao chadema waliunasa kutoka kwenye kompyuta ya Watuhumiwa
hawo, ukionyesha mikakati ya kukihujuma chama hicho pamoja viongozi wa chama
hicho Mwanasheria wa chadema alifafanua na kukanusha ule walaka uliosambazwa
kwenye vyombo vya habari amabapo Zitto kabwe aliusambaza wakati akizungumza na
waandishi wa habari juzi jumapili kwenye hoteri ya serena jijini Dar es salaama
na kusema walaka huo ni tofauti na tulio tumia kumuhukumu kwenye kamati kuu ya
chadema,
“Kuhusu
walaka unaosambazwa na yeye Zitto Kabwe kwenye vyombo vya habari ni
tofauti na ule tuliotumia kumuhukumu kwenye kamati kuu ya chama, na mwenyewe
Zitto anafanya uwongo wa hali ya juu ili kupotosha uma umwamini juu ya kile
anachokisema”alisema Lissu
Vilevile,Tundu Lissu alisema
ukisoma walaka ambao unasambazwa kwenye vyombo vya habari unaonyesha upungufu
wa kiongozi huyo na kusema sababu za uwongo za sisi kumuengua chadema
“Zitto kabwe amewadanganya watanzania kwa
kupia walaka ule nataka niwambie watanzania walaka ule anausambaza nakuonyesha
kamati kuu kuwa tumemuengua chadema kutokana na Hesabu za Vyama vya kisiasa”,
“kutokana nayeye kuwania
nafasi ya mwenyekiti pamoja na ufisadi anausema yeye.Nataka niwambie
wanachadema pamoja na watanzania walaka ambao kamati kuu tumetumia kumuhuku hajazungumzia
hivyo vitu na wala havipo kwenye walaka amabao tumemuhuku na sisi tutahuto
walaka huo mala baada ya siku kumi na nne kupita”alifafanua Lissu
Kuhusu hoja ya ukuguzi wa
fedha ndani ya chadema
Kwa upande waukaguzi wa
matumizi ya fedha ndani ya chadema,Mwanasheria wa chama hicho alisema anayosema
mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto kabwe ni dariri ya uongo anaofanya hivyo kwa
makusudi na akatoa ushahidi kwa waandishi wa habari juu ya ukaguzi wa fedha
ndani chama
“ Mwaka 2010 mkaguzi aliniaviandika vyama vyote
kisiasa vilipie garama ya ukaguzi wa atakaofanya kwenye vyama vya siasa”
Barua hiyo ilisomeka kama
ifuatavyo “mimi sijapewa ruksa ya kukagua ila sijapewa pesa ya kukagu vyama vya
kisias”barua hiyo ilitoka na kwa mkaguzi mkuu wa serikali kwenda kwa vyama vya
siasa
Aidha,Mwanashera huyo wa chadema aliongeza na
kusema mwaka jana mwezi semptemba vilipereka hesabu kwa mkaguzi mkuu wa
serikali pamoja na msajili wa vyama vya kisiasa
“Mwaka jana mwezi semptemba
vyama vitatu vilipereka hesabu kwa msajili wa vyama vya siasa ilonyesha Chama
cha wananchi Cuf walipereka hesabu zao”
“Na chama cha Nccr mageuzi
pia walipeleka pamoja na sisi Chadema,katika ukaguzi ulionyesha vyama viwili tu
ndivyo vilivyofanyiwa ukaguzi ambapo na sisi chadema na Nccr nashamshangaa zito
kabwe anasema chadema haijakaguliwa sijui ananini huyu mtu”alijoji Lissu
Katika hatua nyingine Mwanasheria huyo wa
Chadema alimshutumu aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kuwa
Hajawai kufika kwenye ofisi za chadema tangu achaguliwe kuwa mbunge mwaka 2010
hajawai kufika kwenye ofisi za chama hicho
Kuhusu mgogoro kati ya Zitto
Kabwe na mwenyekiti wa chadema Freemani
HABARI IMEANDIKWA NA MWANDISHI MWANDAMIZI WA BLOG HII, BW.
Na Karoli Vinsent
Na Karoli Vinsent
Hakuna maoni
Chapisha Maoni