DAR CITY YATINGA NUSU FAINALI YA MTOANO WA ROAD TO BAL2027 NAIROBI
Timu ya mpira wa Kikapu ya Dar City leo imefanikiwa kutinga nusu fainali ya mtoano wa Road To BAL2027 baada ya kuifunga Namuwongo Blazers ya Uganda kwa vikapu 91-79 katika mchezo uliyochezwa Nairobi Kenya.
Dar City sasa inacheza mchezo wake wa kukamilisha ratiba wa makundi Novemba 26 dhidi ya Dolphin Basketball ya Botswana na baada ya hapo ndio itasubiria kucheza nusu fainali ya Elite 16 na ikifuzu fainali au ikishinda mechi ya mshindi wa tatu itaenda Afrika Kusini kwa ajili mtoano wa mwisho.

No comments
Post a Comment